Wakati serikali ya Tanzania imeshindwa kusimamia mashirika ya umma
na badala yake kuyabinafisisha, China bado inasimamia na kuendesha huduma
nyingi na kwa ufanisi wa hali ya juu. Picha hizi ni mfano tu wa shirika
la Taxi Mjini Harbin, China. Hii ni kampuni ya serikali ya mji wa Harbin
na kwa huu mji ina idadi ya Taxi zinazofikia 1,200. Hapa zinavyoonekana
kwenye picha, ni wafanyakazi wako kwenye kikao. Tanzania inabidi
tujifunze. Mabasi ya abiria pia yanamilikiwa na kusimamiwa na serikali,
ukiachana na huduma zingine nyiingi. Tanzania tungeweza kubadilika na
serikali ikaweza kusimamia huduma za msingi ingekua chachu ya maendeleo.
Vinginevyo serikali iwe na uwezo wa kutoa tenda ila si kwa asilimia 10
kwani asilimia kumi ndo inayofanya ufanisi usiwepo, pamoja na kupeana
tenda kindugu au kirafiki.
Ubinafsishaji wa Shirika la Usafirishaji Dar es Salaam (UDA) ambao ulizua malumbano kutokana na kugubikwa kwa rushwa hii ikiwa tofauti na wenzetu China ambao wana mpaka mashirika ya Taxi.
..........................................
Kutoka China na Zeph
Post a Comment