Na: Idara ya Habari,MAELEZO
Taasisi
mbalimbali za kidini hapa nchini zilizopata usajili rasmi kwa Mrajis
Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimekanusha kuhusika na tamko
lililotolewa na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Uamsho, Sheikh Mselem Ali la
Waislamu wa Zanzibar wagomee kushiriki katika Sensa ya Watu na Makaazi
Kitaifa inayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo.
Wakizungumza
na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga Wawakilishi wa
Taasisi hizo wamelaani tabia ya Uamsho ya kujipa Mamlaka ya kuzisemea
Taasisi hizo.
Aidha,wameitaka
Jumuiya ya Uamsho kuthibitisha ni kikao gani kilichokaa na kuzungumza
na Taasisi za Kidini na kuamua kwa pamoja kutowa tamko hilo la kupinga
kushiriki kwa Waislamu katika Sensa.
Aidha,
wameihakikishia Afisi ya Mufti na Serikali kuwa watashiriki katika
Sensa ili kusaidia maendeleo ya Zanzibar na kutatua baadhi ya migogoro
ya kijamii na sio kujiingiza katika siasa na kupingana na Serikali kama
ambavyo imekuwa ikifanya Jumuiya ya Uamsho.
Taasisi zimewataka Waislamu kushirikiana na Serikali na kuachana upotoshaji unaofanywa na Uamsho.
Aidha,
wameitaka Jumuiya ya Uamsho kuachana mara moja kutumia kivuli cha umoja
wa Taasisi za kidini Zanzibar wanapoamua mambo yao kwani Jumuiya hizo
nyingi hazikubaliani na Sera yao ya fujo na vurugu.
Mwisho.
Imetolewa na:
Idara ya Habari(MAELEZO) Zanzibar
23/08/2012
Post a Comment