Kumekuwa na mzozo mpya katika
mgodi wa kuchimba madini ya platinum nchini Afrika kusini ambako watu
thelathini na nne walipigwa risasi na kuuawa mapema mwezi huu.
Chama kimoja cha wafanyakazi hao kilichojitenga
mwezi jana , kimewatishia wafanyakazi hao walipokuwa wankuja kazini
asubuhi ya leo.Uongozi wa kampuni hio ya madini ya Uingereza ya Lonmin unaripotiwa kuwa mkutanoni ambako wanafikiria kuifunga migodi yao katika sehemu hio kwa muda.
Wakati huo huo, chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC, kinakutana kujadili migawanyiko juu ya kile kilichotajwa kuwa mauaji ya wafanyakazi wa mgodi wa Marikana , pale polisi walipowaua wachimba migodi thelathini na nne.
Chanzo:BBC Swahili
Post a Comment