Naibu Waziri wa Kazi na Ajira , Dk Makongoro Mahanga akizundua Kozi mbalimbali zinazotazamiwa kutolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kupitia Taasisi yake ya elimu Endelevu ikiwa ni katika mfululizo wa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 20 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tangu kianzishwe mwaka 1992 ambapo jana alikuwa mgeni rasmi.Anaefuatia ni Mkuu wa Taasisi ya Elimu Endelevu,Dk.Kisoza,Pia yumo Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo(Taaluma),Prof.Bisanda na Kaimu Makamu MKuu wa Chuo(RS)Prof,Varisanga(Kulia)
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira , Dk Makongoro Mahanga akiangalia bango lenye kozi hizo baada ya uzinduzi wake hiyo jana katika kituo cha Kinondoni,Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.Taasisi ya Elimu Endelevu iliweza kuzindua kozi mbalimbali zikiwemo za ujasiria Mali wa Biashara ndogondogo.
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Kupitia Taasisi ya Elimu Endelevu walimpatia zawadi Naibu Waziri wa kazi na Ajira,Dk.Mahanga na pichani anaonekana akifurahia zawadi hiyo na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo(Taaluma),Prof.Bisanda.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo(RS),Prof.Varisanga akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Dk.Mahanga baada ya shughuli ya uzinduzi wa kozi fupi zitakazotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kupitia Taasisi ya Elimu Endelevu kuanzia mwaka wa masomo 2012/2013
Washiriki kutoka idara mbalimbali Chuo KIkuu Huria cha Tanzani wakisikiliza kwa makini
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Mahanga akiwa katika picha ya pamoja na Wahadhiri na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania hiyo jana wakati aliposhiriki aktika uzinduzi wa kozi fupi zitakazo anza kutolewa na Taasisi ya Elimu Endelevu kwa mwaka huu wa masomo.
Mama Hassani akiwa kwenye pozi wakati akiandikisha wahudhuriaji waliokuja katika Sherehe hizo zilizofanyika kwa kufna katika kituo cha Kinondoni,ChuoKikuu Huria cha Tanzania akiwa kapozi na wadau wengine wa Taasisi ya Elimu Endelevu.
Wakiwa kwenye pozi la picha kutoka kushoto ni Jacque,akifuatiwa na Lucas Msungu na mdau mwingine ambae jina lake halikufahamika mara moja.
Dk.Benhaji(Kushoto)akiteta jambo na Mr.Neville Reuben kutoka Taasisi ya Elimu Endelevu
Baada ya uzinduzi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Mahanga alipta fursa ya kuongea na waandishi wa habari na kuelezea kufurahishwa kwake na uanzishwaji wa Kozi hizo fupi kwani zitawasaidia wajasiria mali ambao wengi wao hawana maarifa ya biashara pamoja na kozi nyingine zitakazo wasaidia wafanyakazi wa serikali kuongeza ujuzi wao sambamba na kuongeza tija kwa huduma mbalimbali Serikali inazotoa kwa jamii nzima .
Post a Comment