Mabingwa wa klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati timu ya Young Africans
Sports Club, jana jioni ilitembelea Ikulu kuonana na Rais Paul Kagame,
kufuatia mwaliko wa rais huyo wa Rwanda.
Ikiongozwa na mwenyekiti wa Young Africans Sports Club Yusuph Manji,
iliwasili Ikulu ikiwa na wachezaji wake wote walioenda nchini Rwanda
pamoja na viongozi wake.
Mchezaji mpya aliyesajiliwa kutoka APR Mbuyu Twite alikuwa miongoni mwa wachezaji
waliohudhuria dhifa hiyo, ambapo Mwenyekiti wa bodi ya udhamini wa klabu
Mama Fatma Karume na mjumbe wa bodi ya udhamini Seif Ahmed Magari
walimkabidhi jezi ya Yanga rais Paul Kagame.
Kocha Mkuu wa Young Africans Tom Saintfiet na nahodha wake Nadir
Haroub Cannavaro walimkabidhi kombe rais Kagame, kombe la klabu bingwa
afrika mashariki CECAFA ambalo rais Kagame ndio mfadhili wake mkuu.
Young Africans inashuka leo dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Rayon Sports.
Post a Comment