Hata hivyo maswali kadhaa yanapaswa kuulizwa kabla tuseme kuwa wanawake wanaongezeka kwenye ngazi ya uongozi au la.
Kwanza kabisa ni kipi chanzo cha ukandamizaji kwa wanawake? na je wanaweza kukabiliana na hili kwa wao kuwa marais wa nchi?
Ni kitu gani kinachojumuisha kuingia kwa wanawake uongozini Afrika. Wanawake wa Afrika ni wapi? Na hususan zaidi, wanawake hawa wanaochukua uongozi je ni wawakilishi wa wanawake Afrika?
Utafiti unaonyesha wazi kwamba kiini cha ukubwa wa mwanamume ni chanzo cha ukandamizaji wa wanawake wengi Afrika.
Ili wanawake waweze kuongezeka katika ngazi za uongozi, fikra ya kuwaona wanaume kuwa bora zaidi ni lazima ifutike.
Kutokana na uhusiano huu wa kijinsia, mtu huwaza je mwanamke kuchukuwa uongozi wa taifa hususan ikizingatiwa upendeleo uliopo wa jinsia moja katika taifa lenyewe, kutaleta mabadiliko?
Rais wa Malawi Joyce Banda
kuna dhana kwamba hadi mtu atakapobadili mfumo unaompendelea mwanamume, mwanamke kujiunga katika uongozi wa taifa huishia kuwa mmoja wa wanaume na mfumo humlazimu kuwa kama mwanamume. Malawi
Na kwa hakika ili kudumu katika uongozi huo ni lazima awe na uwezo wa kutekeleza majukumu kama mwanamume na alihakikishie taifa kuwa ataendelea kuwatukuza wanaume.
Suala jingine muhimu kukumbuka ni kuwa hivi sasa ni nchi mbili pekee kati ya 54 Afrika zinaongozwa na wanawake.
Mizani hii iliyoegemea upande mmoja kwa wengine wanaitazama kuashiria kuongezeka kwa wanawake katika uongozi.
Kwa mujibu wa ripoti ya kongamano la uchumi duniani mwaka 2011 pengo la kijinsia linaashiria kuwa nchi kumi kati ya ishirini na moja zilizo na kiwango kikubwa cha ukosefu wa usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume zipo Afrika.
1. Chad, kiwango duniani: 134
2. Mali, kiwango duniani: 132
3. Ivory Coast, kiwango duniani: 130
4. Morocco, kiwango duniani: 129
5. Benin, kiwango duniani: 128
6. Egypt, kiwango duniani: 123
7. Algeria, kiwango duniani: 121
8. Nigeria, kiwango duniani: 120
9. Cameroon, kiwango duniani: 119
10. Ethiopia, kiwango duniani: 116
kati ya nchi 135
Hili ni jambo la kuchekesha hususan mtu anapokumbuka kuwa wanawake wanajumuisha zaidi ya nusu ya idadi watu katika nchi nyingi Afrika.
Ili wanawake kuonekana kuchukua uongozi , chochote atakachofanya ni lazima kishuke kwa mwanamke mwenzake.
Hili lina maana kuwa ni lazima tubadili mifumo ya kikoloni iliyoidhinishwa kwa jamii ya Afrika kama vile kuendelea kwa mataifa, dini zilizopangwa, kuunda upya taasisi zinazowapendelea wanaume na zinazowakandamiza wanawake katika viwango binafsi na vya kijamii kama vile katika ndoa.
Tunaposema wanawake wanachukua uongozi tunapaswa kuwa na uhakika iwapo tunazungumzia uongozi au ni katika muundo.
Kuubadili muundo kutawawezesha wanawake kuinuka kutoka mashinani badala ya kuteuliwa.
Mabadiliko yanahitajika lakini hili linaweza tu kufanyika iwapo mfumo mzima utabadilika.Idadi kubwa ya wanawake ni maskini, wanaoishi mashambani na ambao hawakusoma.
Mkuu wa tume ya muungano wa Afrika Nkosazana Zuma
Mtu anaweza kuuliza vipi tunaweza kuhakikisha kwamba wanawake wanainuka kikweli Afrika.
Botswana na Rwanda ni mifano ya nchi ambazo zinashuhudia ongezeko muhimu la kushirikishwa wanawake katika uongozi wa kisiasa.
Uhamasisho wa kusisitiza usawa wa kijinsia ni jambo linaloshughulikia ukosefu wa usawa katika taasisi na sio kuwa na mwanamke mmoja pekee anayeiendesha serikali.
Wanawake wanahitaji kuwa katika ngazi za uongozi katika bodi tofauti, vyama vya kisiasa na nafasi za kukuza elimu kama vile vyuo vikuu na kadhalika.
Iwapo tunaweza kupata asilimia 50 ya bodi na bunge zilizo na wanawake basi tutafungua nafasi kutoka mashinani hadi ngazi za juu, badala ya kuwa na mwanamke mmoja katika ngazi ya juu kwenye taasisi ambayo haipendelei wanawake.
Rais mwanamke anaweza kufanya mabadiliko makubwa katika nchi yake na hili linaweza kuwa katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika demokrasia kuhakikisha kuwa wanawake wana uwezo katika taifa.
Atahakikisha kuwa sauti zao hususan ile ya mwanamke ambaye amekosa elimu, anayeishi mashambani na hakusoma, zinazingatiwa na hazidunishwi kwa kudharauliwa au kukosa kupewa nafasi ya kujieleza.
Rais mwanamke anaweza kushughulikia masuala yanayowahusu wanawake.
Lakini kiongozi huyo anapaswa kukumbuka kuwa fikra ya mwanamume ndiye mwenye uwezo, hutumika kudhibiti rasilimali na uongozi, na iwapo fikra hii itatishiwa, basi mbinu mpya huundwa zitakazomkumbusha kiongozi mwanamke kwamba ataadhibiwa na wale wanaonufaika kwa fikra hii, iwapo yeye kama mwanamke hatoliendeleza hili.
Kwa hiyo rais mwanamke anapswa kuzingatia kwa ukubwa haki ya kijinsia.Anapswa kuwa mtu ambaye msimamo wake wa kisiasa unajumuisha kuwepo kwa maadili ya kiwango cha juu, ukweli na haki .
Na je huenda rais mwanamke asijihusishe katika vita. Msimamo huu huenda ukawa na athari kubwa kisiasa na matokeo yake huchukua muda kutambulika.
Kiongozi wa aina hiyo anafahamu kwamba mabadiliko sio tukio ni hatua na faida ya kuwepo upendeleo kwa wanawake itakuwepo katika siku za usoni na watu wengine.
Rais mwanamke atashughulikia masuala ya kiuchumi kwa njia ya busara, kwa mpangilio na makini ya kujua kufanya hivyo kwa kuwa anafahamu kwamba umaskini hutoa njia za kusababisha na kushinikiza ukandamizaji dhidi ya wanawake kama vurugu za kijinsia, vifo vya akina mama wakati wa kujifungua , Kusambaa kwa virusi vya ugonjwa hatari wa ukimwi na madhara ya mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.
Mwanamke anaweza kuonyesha kwamba anatambua wanawake wengi wamo kwenye mfumo wa kibinafsi na wanaishi katika hali dhaifu.
Mtu anaweza kuuliza je taifa lisilo tawaliwa na wanaume lina sura gani?
Kwanza taifa litatilia mkazo wanawake kushiriki katika taasisi tofauti, katika viwango tofauti hususan katika masuala yanayowahusu wanawake.
Taasisi zinazotoa nafasi za uwezo wa kisiasa zitabadilishwa kuwakaribisha na kuwaweka wanawake katika viwango vikubwa kuanzisha na kubadili mbinu za kuliendesha taifa linalopendelea mifumo ya utawala wa wanaume.
Taifa kama hilo litaidhinisha mfumo wa kike katika kuleta maendeleo na kukabiliana na umaskini, vifo vya akina mama wakati wanapojifungua, kupambana na virusi vya ugonjwa hatari wa ukimwi na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ni vizuri kuwa idadi ya wanawake waliomo uongozini Afrika inaongezeka, lakini kwa hili kuweza kushirikisha ongezeko katika kumuelezea mwanamke na maisha anayoishi Afrika, muundo unaomuunda mtu, awe ni mwanamume, mwanamke, na pia uongozi, unapaswa kubadilika.
Baada ya hapo tunaweza kuanza kuuliza iwapo kuibuka kwa wanawake kama Joyce Banda, kuna maana kwamba wanawake wanaochukua uongozi wanaongezeka. Je nini maoni yako? Jiunge na mjadala!
Chanzo:BBC Swahili
Post a Comment