VIGOGO WAWAHENYESHA VIJANA, WENGI WARUDI, MASHA, MWAKALEBELA WAINGIZWA KUNDINI
Waandishi Wetu Dar na mikoani
KINYANG'ANYIRO cha kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinazidi kupamba moto huku matokeo yakionyesha kuwa vigogo wa chama hicho wameibuka kidedea.
Katika uchaguzi huo ulioanza juzi katika wilaya kadhaa nchini, watu maarufu ndani ya chama hicho wakiwamo waliokosa ubunge katika uchaguzi uliopita waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali wameshinda.
Uchaguzi huu unachukuliwa na chama hicho kama sehemu ya kupanga safu ya uongozi ambayo itatumiwa na chama hicho kutetea kuendelea kupata ridhaa ya kuongoza nchi.
Rais Jakaya Kikwete wakati akifungua kikao cha Halmashuari Kuu (Nec) mjini Dodoma hivi karibuni alisema kuwa wameamua kupitisha majina ya vijana wengi ili wapate timu ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Iringa Mjini
NEC: Katika nafasi hiyo Mahamoud Madenge alishinda kwa kupata kura 281, huku akiwabwaga Vitus Mushi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Enock Ugulumo na Michael Mlowe.
Nafasi ya Mkutano Mkuu wa Taifa: Katika nafasi hiyo ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela aliibuka kidedea.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa CCM Iringa mjini, Msimamizi wa Uchaguzi huo, Daudi Yasin aliwataja wengine walioshinda nafasi hiyo inayohitaji wajumbe watano kuwa ni Salim Abri (Asas) Diwani wa Viti Maalumu, Agusta Mtemi, Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi na Fatuma Ngole.
Mwenyekiti: Mwenyekiti wa zamani wa CCM Wilaya Iringa Mjini, Abeid Kiponza aliibuka mshindi na kutetea nafasi yake huku akimshinda mpinzani wake ambaye ni
Katibu Mkuu wa Soka Mkoa wa Iringa, Eliud Mvela.
Aliwataja wajumbe wawili wa halmashauri kuu kundi la wazazi kuwa ni Alli Mbaya na Shadrack Mkusa.
Walioshinda nafasi hiyo kundi la wanawake ni Nikolina Lulandala ambaye ni Diwani wa Kata ya Gangilonga, Ashura Jongo na Halima Msanya.
Upande wa vijana walioshinda ni Ally Simba, Salum Kaita, Mwaija Mwinyikayoka na Crala Shirima.
Kwa upande wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa, wagombea wawili ambao ni Zainab Kufakunoga na Chiku Masanja ambaye ni Katibu wa Umoja wa Wanawake, Iringa mjini walipita bila kupingwa.
Songea Vijijini
Nec: Mwanasheria wa CCM makao makuu Dodoma, Glorius Luoga alishinda nafasi ya Ujumbe wa Nec katika Wilaya ya Songea Vijijini.
Mwenyekiti: Akitangaza matokeo hayo jana Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo Mwenyekiti wa UWT Mkoa Ruvuma, Mariam Yusuph alisema nafasi ya Mwenyekiti imechukuliwa na Nelly Due.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa: Aliwataja walioshinda nafasi ya ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa ni Joseph Muhagama, Vastus Mfikwa, Athon Kantala,Celina Kayombo na Rajab Mtiula.
Songea Mjini
Nec: Kwa upande wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Msimamizi wa Uchaguzi huo, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho alimtangaza Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mshindi wa Mjumbe wa Nec.
Mwenyekiti: Nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya imechukuliwa na Gerod Muhenga.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa: Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ni Anusiatha Ngatunga, Andrew Chatwanga , Charles Muhagama, Consolatha Kilowoko na Mathias Nyoni.
Nyamagana
Nec: Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha ameibuka kidedea akiwashinda wapinzani wake, Biku Kotecha na James Bwire katika uchaguzi wa mjumbe wa Nec baada ya kuwashinda washindani wake.
Mwenyekiti: Kada wa siku nyingi wa CCM, Raphael Shilatu ameshinda nafasi hiyo akiwashinda washindani wake, Yahya Nyaonge, Joseph Bupamba na Mashaka Kaguna.
Ilemela
Nec: Nafasi ya Ujumbe wa Nec aliyechaguliwa ni Israel Mtambalike akiwashinda washindani wenzake, Nashon Kennedy, Mafuru Eliazar na Ahnes Kingu.
Mwenyekiti: Katika uchaguzi wa mwenyekiti, Nelson Mesha aliibuka kidedea akiwashinda wenzake.
Morogoro Mjini
Nec: Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameibuka mshindi wa nafasi hiyo.
Mwenyekiti: Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Fikiri Juma ametetea chama hicho baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana.
Mjumbe afa katika ajali Chunya
Uchaguzi wa CCM, Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya umeingia dosari baada ya wajumbe wa mkutano mkuu, kupata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja, Isaya Nchimbi (45), ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha Tawi la Madimbwini Kata ya Mamba na wengine 92 kujeruhiwa.
Taarifa zilizopatikana kutoka eneo la tukio zinadai kuwa ajali hiyo ilitokea jana, saa 2:30 asubuhi katika Kata ya Matundasi , baada ya dereva wa gari hilo aina ya Fuso, kudaiwa kupokea simu iliyokuwa ikiita mfukoni, huku gari hilo likiwa kwenye kona hivyo kumshinda na kupoteza mwelekeo na baadaye kupinduka.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya, Dk Heny Mwansasu, amethibitisha kutokea majeruhi wa ajali hiyo ambayo imesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 92 kujeruhiwa , ambapo walifikishwa hospitalini hapo saa 4 asubuhi.
Dk Mwansasu alisema kati ya majeruhi hao, 11 hali zao ni mbaya na 84 walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kwa kuwa wengi wao walipata mshtuko na wengine majeraha madogomadogo.

Chanzo:Mwananchi
Post a Comment