Kuna mvutano na wiwasi katika mji wa Pibor, Sudan Kusini, karibu na mpaka wa Ethiopia.
Shirika
la kimataifa la msaada wa matibabu, MSF, limewaondosha wafanyakazi wake
wa kigeni na wengi walio wenyeji wamekimbilia vichakani.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika
Sudan Kusini, Hilde Johnson, amesema hali katika mji wa Pibor ni ya
wasiwasi, na kuna ripoti kuwa wakaazi wamekimbilia vichakani.
Kuondoshwa kwa wafanyakazi wa MSF kumewaacha watu kama 90,000 bila ya huduma za afya.
Tisho linatokana na kiongozi wa wapiganaji, David Yauyau, ambaye amewavutia vijana wa kabila la Murle.
Inaarifiwa kuwa wenyeji wamekerwa na wanajeshi
wa serikali ya Sudan Kusini waliowekwa kwenye eneo hilo, wengi wao
kutoka kabila la maadui wao la Nur.
Inasemekana wanajeshi hao wamewapiga na kuwabaka baadhi ya wenyeji.
Umoja wa Mataifa unasema unafuatilia hali hiyo
kwa makini na uko tayari kutuma askari zaidi kujumuika na kikosi cha
kusimamia usalama kilioko mjini Pibor chenye askari 80.
Mwaka jana maelfu ya watu wa kabila la Nur waliwashambulia Wamurle huko Pibor na kuuwa watu kama 150.
Mapigano kuhusu ng'ombe na wanawake yanatokea mara kwa mara Sudan Kusini.
Via BBC Swahili
Post a Comment