Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AZINDUA UJENZI WA JENGO KUU LA ELIMU HURIA NA MASAFA

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Prof.Tolly Mbwette akitoa maelezo ya awali kuhusiana na ujenzi wa Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa kwa Wageni waalikwa katika uzinduzi waliokuja kushuhudia Uzinduzi huo leo 5/9/2012 katika Ofisi za Muda za Chuo Kinondoni,Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Prof.Samuel Wangwe akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk.Shukuru Kawambwa(Mb) ili kuzindua ujenzi wa  Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk.Kawambwa akifurahi baada ya kuzindua ujenzi wa Jengo kuu la Elimu Huria na Masafa leo huku Mama Maria Nyerere akimpongeza.
 Mama Maria Nyerere,Mhe.Dk.Kawambwa wakifurahia jambo na wageni wengine baada ya uzinduzi  wa Jengo 
 Wakifurahia jambo kabla ya kuanza kupanda juu ya ghorofa kukagua ujenzi huo.
 Makamu MKuu wa Chuo,Prof.Mbwete akimpa maelezo namna Chuo kitakavyolitumia jengo hilo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk.Kawambwa anaesikiliza kwa makini kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo,Prof.Samuel M.Wangwe.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dk.Kawambwa akiteta jambo na mafundi wakuu wa Kampuni inayojenga Jengo hilo toka nchini China.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa(kushoto) akishuka ngazi baada ya kukagua ujenzi wa Jengo hilo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzani,Prof.Mbwette

 Baada ya uzinduzi na kukagua ujenzi huo wageni walipata picha ya pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Shukuru Kawambwa pamoja na Mama Maria Nyerere aliyekuwepo katika uzinduzi huo.
 Jengo la kuu la Elimu Huria na Masafa kama linavyoonekana ambalo ujenzi wake umezinduliwa leo 5/9/2012 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk.Kawambwa

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top