AZAM FC tayari wapo mjini Mbeya, kwa ajili ya yao ya Jumatano, dhidi ya wenyeji Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Timu hiyo imewavutia wakazi wengi wa mji wa mbeya na wamekuwa wakijaza watu kila sehemu inapoonekana timu hiyo jana katika viwanja vya shule ya Iyunga palikuwa hapatoshi wakati timu hiyo ikifanya mazoezi.
AZAM FC leo jioni watafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, ili kuuzoea kabla ya mechi ya kesho dhidi ya wenyeji, Prisons katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi na washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame wapo mjini Mbeya tangu juzi saa 1:00 usiku na jana walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa sekondari ya Iyunga mjini humo.
Kikosi kizima cha Azam kipo vizuri kuelekea mchezo unaitarajiwa kuwa mgumu kwao na wachezaji wa morali ya ushindi, ili kuweka vizuri mazingira ya kutwaa taji la kwanza la ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara.
Azam waliondoka Morogoro juzi asubuhi baada ya mechi yao na Polisi kwenye Uwanja, Jamhuri Jumamosi ambayo walishinda 1-0, bao pekee la mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
Mechi nyingine Ligi kuu Bara ni kati ya Simba na Kagera,Uwanja wa Taifa
Polisi Vs Ruvu Shooting,JKT Mgambo v Toto African,Uwanja wa Mkwakwani,JKT Oljoro Vs African Lyon Arusha.
Chanzo:moronew.blog
Post a Comment