Siku chache baada ya kushindwa amri kumi za Yanga na kufangasha virago Mbelgiji Tom Saintfiet amepata ulaji wa kuifundisha timu ya Taifa ya Yemen.
Sainfiet aliyepokelewa kifalme wakati anakuja nchini kufundisha Yanga aliifundisha Yanga kwa siku zisizozidi 80.
Pia itakumbukwa kuwa aliweka rekodi ya kushinda michezo 14 na kupoteza 2 tu huku akiwaachia taji la Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame.
Kipigo dhidi ya Mtibwa Sugar cha goli 3-0 bila ndicho kilichoivisha safari yake ya kuondoka Jangwani.
Saintfiet, Kabla ya kuja Yanga aliwahi kuwa kocha wa Ethiopia.
Yemen ataanza kazi siku ya Jumamosi na ataiongoza timu yake mpya dhidi ya Lebanon katika mechi ya kirafiki iliyopangwa kufanyika Oktoba 16 ikiwa ndio mechi yake ya kwanza na atapata wasaa mzuri wa kuiangalia vizuri timu hiyo ya Yemen.
Post a Comment