Wengine waliamua kuucheza kabisa sio kuangalia tu walivyokuwa wanaimba na kucheza tu hapo ni kwa nafasi kila mtu na yake ili kuweza kuikonga nyoyo kutokana na muziki huo wa injili uliokuwa unaporomoshwa na Flora mbasha.
Flora Mbasha(mwenye gauni rangi ya bluu) akiwajibika vilivyo jukwaani na Kwaya yake huku umati huo ukimsindikiza nao kwa kucheza
Unaweza kusema yuko chini ya Ulinzi moja kwa moja Kituoni La hasha hapo yuko matembezini mtaani lakini huko Kongo kutokana na hali ya usalama ilivyo walipewa Ulinzi wa kutosha hivyo muda wote waliokuwa Kongo.Emmanuel Mbasha akiwa ameongozana na Askari ambao walihakikisha wana kuwa salma muda wote.
Si gwaride tu Hata Muziki nimo !!! Haikujulikana Jamaa huyu (Kushoto) ambae ni askari alisahau lindo lake kwa muda au ni utamu wa neno la Mungu lililotolewa kupitia muziki wa injili kutoka kwa Flora na Emmanuel Mbasha waliokuwa Kongo kwenye tamasha kiasi cha kushindwa jizuia na kujumuika jukwaani.
Katika Tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na Watu wengi wakazi wa Goma na Vitongoji vyake. Vilipelekea Jeshi la Congo kuingia Kazini kwa ajili ya Ulinzi wa Wanamuziki hao kila walipokuwa wanakwenda ili kuwaepusha na fujo za furaha za Wakazi wa Congo.
Flora na Emmanuel Mbasha ambao juzi kati wametoka Katika Nchi ya Marekani na Sasa Wako Congo, na baada ya hapo Watakuwa Wakijipanga na Trip zingine za Nje ya Nchi.
Flora na Emmanuel Mbasha ndio Wanamuziki Pekee wa Injili Tanzania ambao wiki chache zilizopita walionesha Moyo wa Shukrani kwa Media za Tanzania kwa Kutambua Mchango wa Vyombo Vya habari Vya Kikristo na Vile Mchanganyiko Maalum.
Big Up Emmanuel na Flora Kwa Kuwakilisha Vema Tanzania.
Chanzo:Paradise Today.
Post a Comment