Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BURUNDI YAINYOA TANZANIA BARA

 John Bocco akimtoka beki wa Burundi 

Burundi wanaendelea kuongoza kundi B wakiwa na pointi 6 wakifuatiwa na Tanzania Bara na  Sudan zenye 3 kila moja baada ya kushinda mechi moja.
Pamoja na kufungwa bado matumaini ya Tanzania Bara  kuendelea robo fainali yapo kutokana na point 3 ilizozitia kapuni mchezo wa kwanza dhidi ya Sudani.

Mpira unaingia dakika 4 za nyongeza huku Burundi wakicheza kwa kubutia tu mpira bora liende.

Dak 80: Tanzania Bara 0-1 Burundi zimebaki dakika kumi 

DK 77:Tanzania Bara 0-1 BURUNDI
Dak 74: Kadi ya njano kwa Kelvin Yondani baada ya kumpakibega mchezaji waBurundi aliyekuwa anajaribu kuipenya ngome ya Tanzania Bara

Dak 68: Mwinyi Kazimoto anashindwa kuendelea na mchezo nafasi yake inachukuliwa na Shaaban Nditi 

Dak 63: Mwinyi Kazimoto anagalagala chini baada ya kuchezewa faulo mbaya naMchezaji wa Burundi ambae anazawadiwa kadi yaNjano.

Dak 53, Issa Rashid anaingia kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe alieumia wakati anajaribu kumzuia Ndikumana

Dak 52, Goal:BURUNDI wanapata bao kwa njia ya penati Suleimani Ndikumana anaifungia goli Burundi Tanzania Bara 0-1 Burundi (Ndikumana) 

Dak 49: Penati: Burundi wanapata penati baada ya Shomari Kapombe kufanya madhambi kwa kumkwatua Selemani Ndikumana ndani ya penati.

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza kipindi cha pili 

Halftime: Tanzania Bara 0-0 Burundi 
 Wachezaji  wa Burundi wakimuweka chini ya Ulinzi mkali John Bocco ili asilete madhara katika lango lao.Picha na BongoStaz Blog.

Dak 45: Zimeongezwa dakika 2 

Dak 42: Kadi ya njano kwa Amir Maftah 

Dak 41: Mchomo wa Amri Kiemba unaokolewa na golikipa wa Burundi 

Dak 36: Simon Msuva anatoka na anaingia Amri Kiemba 

Dak 30:Tanzania Bara 0-0 Burundi 

Dak 27: Simon Msuva anapiga staili ya ndizi toka nje ya eneo la hatari lakini golikipa anaunyaka mpira 

Dak 20: Tanzania Bara 0-0 Burundi

Dak 6: Simon Msuva anapoteza nafasi ya wazi baada ya kubaki yeye na kipa 

Kilimanjaro Stars vs Burundi. Mchezo umeanza

Kikosi cha Tanzania Bara kinachoanza: Kaseja, Nyoni, Maftah, Kapombe, Yondani, Domayo, Ngassa, Abubakar, Bocco, Kazimoto, Msuva

author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top