Treni za zamani Kenya
Shirika la reli nchini Kenya limezindua
treni mpya ambayo ina mwendo wa kasi ili kutoa huduma kwa wakaazi wa
viungani mwa mji wa Nairobi.
Ni treni ya kwanza ya aina yake kuzinduliwa tangu Kenya kujipatia uhuru mwaka 1963. Treni hiyo inanuiwa kupunguza msongamano wa magari mjini Nairobi ambao ni mojawapo ya miji unaokuwa kwa kasi barani Afrika ukiwa na watu zaidi ya milioni thelathini.
Rais Kibaki aliyefungua rasmi kituo hicho, alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuipanda treni hiyo.Kituo cha treni cha Syokimau ni cha kwanza cha aina yake nchini Kenya, kikiwa na mashine za elektroniki zinazokagua vyeti vya usafiri, pamoja na skirini kubwa ambazo zinatangaza safari za treni.
Wateja wanafurahia usafiri kwani viti vya treni hizo ni vya nguo ikilinganishwa na hli ilipokuwa zamani.
Kila behewa lina uwezo wa kubeba abiria sabini pamoja na miamoja na ishirini watakao simama. Huduma hiyo itakuwa ya kasi na bora zaidi ikilinganishwa na treni za hapo nyuma na pia zitatumia njia tofauti ya reli.
Safari ya kutoka mtaa wa Syokimau inachukua dakika kumi na tano kwa treni hizo huku ikiwa mtu atakwenda kwa gari itamchukua hata masaa mawili. Itamgharimu abiria shilingi miambili kwenda na kutoka mjini.
Post a Comment