KWA mujibu
wa ripoti za Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya wanaume ambao
wanakuwa wanaume suruali inazidi kuongezeka kwa kasi huku kukiwa hakuna
dalili za kupungua kwa tatizo hilo.Sababu kubwa kwa sasa ni kukua kwa
matumizi ya vyakula vya viwandani. Vyakula hivi kwa bahati mbaya huwa
vina kemikali nyingi.
Hakuna shaka kwamba hata wewe umekuwa shahidi, kwa mfano maji mengi
yanayouzwa siku hizi yamesafishwa kwa kemikali, juisi nyingi
hazijatengenezwa kwa matunda halisi, bali zimetokana na harufu ya
matunda na kemikali.
Ulaji usiofaa unaonekana kuwa ni mojawapo ya sababu kubwa za wanaume
kwa wanawake kusumbuliwa na tatizo la nguvu au uwezo katika kushiriki
jambo hili.
Ingawa tatizo la upungufu wa uwezo huo linaonekana zaidi kwa wanaume,
hata wanawake nao wanasumbuliwa nalo, kwa maana ya kukosa hamu ya
kushiriki tendo la ndoa.
Hata hivyo tiba ambayo wanaume wanaweza kutumia, ni ile ile ambayo
wanawake wanapaswa kuitumia, kwa maana ya kula aina fulani ya vyakula
ili nao waweze kuwa sawasawa kama walivyo watu wengine.
Wengine wanakula tu ili mradi tumbo limejaa, bila kuangalia hiki nakula kwa ajili ya kwenda kufanya nini katika mwili.
Mafunzo mengi yametolewa kuhusu vyakula kuanzia shule za msingi hadi
sekondari na vyuo, kwamba mayai yanasaidia nini, vyakula vyenye kuongeza
nguvu, wanga nk ni vipi. Lakini bado si wengi wanaojali
walichofundishwa.
Pombe inasaidia nini katika mwili? Sigara inasaidia nini katika
mwili? Kahawa, soda na vyakula unavyotumia vina msaada gani mwilini? Ni
mambo ambayo unapaswa kuyajua.
Ndugu yangu acha tabia ya kula tu vitu ili mradi unashiba.
Unaharibu mwili wako, kwani baadhi ya vyakula vinachangia ugonjwa wa
kisukari au magonjwa mengine mwilini kama moyo au nguvu za kiume
kupungua hasa vile vya jamii ya mafuta.
Hata matumizi ya mafuta ya kula ni lazima kuwa nayo makini, kuna
baadhi ya mafuta yanachangia mirija ya kupitisha damu katika mwili
kuganda, matokeo yake damu haipiti vizuri, kitendo ambacho kinachangia
mwili wa mwanadamu kuwa dhaifu.
Wengi ni wazuri wa kusoma na kushukuru kwa mada nzuri, lakini hilo
silo ninalotaka; ninachotaka ni kuona mtu anachukua hatua ili kuleta
mabadiliko.
Viko vyakula maalumu vilivyotengenezwa tayari kwa ajili ya kuondoa
tatizo la nguvu za kiume, lakini unaweza kujaribu kutumia baadhi ya
vyakula kama tangawizi vina msaada katika mwili.
Kitaalam, tangawizi ni moja ya vyakula vinavyoweza kurejesha nguvu za
kiume; Jinsi ya kufanya ni kwamba unaweza kuichemsha tangawizi na
ukatumia kwa kuinywa kama chai asubuhi, mchana na jioni.
NJIA NYINGINE YA KUFANYA:
Unaweza pia kuchukua kitunguu saumu kisha changanya na asali pamoja na mmea fulani unaitwa habat soda na uwe unakunywa mchanganyiko huo mara tatu kwa siku.
Ugali wa mtama asilia, mchuzi wa matembele, pweza, mrenda na maziwa navyo vina msaada katika mwili wa mwanadamu.
Mambo yanayochangia kuwa na nguvu imara ni mawili nayo ni kula
chakula bora pamoja, kupata mahitaji muhimu ya mwili na kisaikolojia
unahitajika uwe na amani.
Ukiwa na hofu japo kidogo tu, au msongo wa mawazo hata mwanamke wako afanyeje kukuliwaza ni ngumu kusisimka ipasavyo.
Katika kushiriki jambo hili la ndoa, unapaswa kuwa katika mazingira na muda ambao unajisikia huru.
Zaidi ya yote pendelea kunywa maziwa yaliyo changanywa na asali
mbichi, kunywa maji mengi, punguza kula vitu vyenye sukari, na kula
matunda, mboga za majani kwa wingi.
Pendelea kufanya mazoezi ya viungo, jizoeshe kutembea kwa miguu au kutumia baiskeli angalau nusu saa kwa siku.
Kama unakunywa pombe acha kabisa, punguza mawazo pale unapokuwa na matatizo, elewa kuwa matatizo ni sehemu ya maisha.
Somo hili kwa Hisani kubwa Ya Jukwaa Huru
Post a Comment