Klabu ya Yanga leo imesaini makubaliano ya upembuzi akinifu na kampuni
ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China,
juu ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa Kaunda katika eneo la makao
makuu ya klabu Jangwani
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji amesema wamefikia
hatua hiyo baada ya kukaa uongozi na kamati ya utendaji na kujadili juu
ya hatua hiyo ambayo kampuni ya BCEG itaanza kazi wiki ijayo na pindi
watakapokalmilisha michoro zoezi litakalofuata litakua awawu ya ujeni
wenyewe.
Hiki ni kipindi cha kufanya shughuli za kimaendeleo,m na
hasa kipindi hichi ambacho klabu yetu ipo katika amani namshikamano kwa
viongozi na wanachama, hivyo naamin mara tutakapomaliza suala la uwanja
tutaanza pia ujenzi wa jengo lakitega uchumi mtaa wa mafia alisema
'Manji'.
Naye Mkurugenzi wa shirika la BCEG nchini, bwana Geng
Hijuan amesema amefurahi kufikia hatua hiyo na klabu ya Young Africans,
kazi waliyopewa sasa wataifanya kwa uhakika mzuri na kutoa makadirio
halisi juu ya gharama ambazo zitagharimu kufanikisha mradi huo.
Kampuni
ya BCEG kutoka nchini China ndiyo iliyojenga uwanja wa Taifa wa kisasa
jijini Dar es salaam na sasa ndio waliopewa kazi ya ujenzi wa Uwanja wa
kisasa wa Kaunda.
Naye makamu mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement
Sanga amemseama, makadirio ya uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua
watazamaji elfu thelathini (30,000) mpaka elfu arobaini (40,000)
kutegemea na wataalam watakavyoona, pia utakua na huduma zote za muhim
katika viwanja vya kisasa.
Manji alisema mategemeo ya Kamati ya
Utendaji ni kuanza kujengwa kwa uwanja huo mapema kabla ya mwezi juni
mwakani, ambapo desemba 8 mwaka huu watasubiria kupata baraka za
wanachama katika mkutano mkuu.
Chanzo:Yanga
Post a Comment