Rais Mohamed Morsi amesisitiza Ijumaa
(22.11.2012)kuwa Misri inaelekea katika "uhuru na demokrasia",baada ya
kujilimbikizia madaraka makubwa,hali ambayo imezusha mapambano kati ya
wale wanaomuunga mkono na mahasimu.
"Uthabiti wa kisiasa, uthabiti wa kijamii na uthabiti wa kiuchumi ndio
kitu ninachokitaka na ndio ninachokifanyia kazi," ameuambia mkusanyiko
wa wafuasi wake nje ya Ikulu ya nchi hiyo.
Wapinzani wa Morsi walianza hatua ya kukalia eneo la Tahrir kwa muda wa
wiki moja, eneo ambalo linatambulika kuwa ishara ya maandamano ambayo
yameuangusha utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak mwaka
jana, na wametoa wito wa maandamano makubwa zaidi siku ya Jumanne.
Magari yachomwa moto
Mapambano yalizuka kati ya polisi na waandamanaji karibu na uwanja huo,
huku waandamanaji wakichoma moto gari la polisi, wamesema watu
walioshuhudia.
Na mapambano ya ghasia yamezuka kati ya waungaji mkono wa Morsi na
mahasimu wao katika mji wa Suez pamoja na mji wa Alexandria , ambapo
waandamanaji walivamia ofisi ya chama tawala cha udugu wa Kiislamu.
Katika tamko ambalo lilisomwa katika televisheni siku ya Alhamis, rais ,
"anaweza kuchukua uamuzi wowote ama hatua yoyote kulinda mapinduzi.
Maamuzi ya kikatiba, maamuzi na sheria zinazotolewa na rais ni za mwisho
na haziwezi kukatiwa rufaa."
Hatua hiyo ni pigo kwa vuguvugu la wanaopendelea demokrasia ambao
walifanikisha kumuondoa madarakani rais Mubarak , na kuzusha hofu kuwa
Waislamu wanaweza kujikita zaidi katika madaraka.
Jumuiya ya kimataifa yaingiwa na wasi wasi
Pia hali hiyo imezusha wasi wasi kimataifa, huku Marekani ikitoa wito wa utulivu na kuzitaka pande zote kufanyakazi kwa pamoja.
"Uamuzi na matamko yaliyotangazwa Novemba 22 yamezusha wasi wasi kwa
wengi wa Wamisri na jamii ya kimataifa, amesema msemaji wa wizara ya
mambo ya kigeni ya Marekani Victoria Nuland.
"Moja kati ya nia ya mapinduzi ilikuwa kuhakikisha kuwa madaraka
hayatakuwa mikononi mwa mtu mmoja ama taasisi," amesema msemaji huyo wa
wizara ya mambo ya kigeni katika taarifa.
Mjini Brussels, msemaji wa mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa
Ulaya Catherine Ashton amesema, " Ni muhimu sana kwamba hatua za
kidemokrasia zikamilike kwa mujibu wa jukumu linalochukuliwa na uongozi
wa Misri."
Shirika linalotetea haki za binadamu la Amnesty International
limeshutumu madaraka hayo mapya ya Morsi, ambayo "yanakandamiza utawala
wa sheria na kuileta enzi mpya ya ukandamiza."
Waandamanaji mjini Cairo
"Watu wanaunga mkono uamuzi wa rais," kundi la watu lilikuwa likiimba.
Siku ya Alhamis, (22.11.2012) Morsi aliipunguzia madaraka mahakama
ambayo inapingana nae, ambayo imekwishafikiria iwapo kuondoa jopo
linalodhibitiwa na kundi hilo la Waislamu ambalo linaunda rasimu ya
katiba , na kuwavua madaraka majaji ya haki ya kutoa hukumu juu ya kesi
ama kupinga uamuzi wake.
Post a Comment