Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

KENYATTA NA RUTO WAUNGANA RASMI


Wanasiasa wawili wa Kenya wanaotaraji kugombea uongozi na ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa wanaungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika mkutano wa hadhara uliofanywa mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea mwenza wa Bwana Kenyatta.
Siku ya Ijumaa shirika la Kenya la kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha kesi mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka.
Wanasiasa wengine maarufu wa Kenya piya wameshtakiwa na ICC.

Chanzo:www.bbc.co.uk/swahili
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top