Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAZIRI MUHONGO AMTOLEA UVIVU PROF.LIPUMBA

*Asema anapotosha umma kuhusu mgawo wa umeme
*Awataka vijana kuchapa kazi badala ya siasa
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amemtolea uvivu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kauli yake aliyoitoa kuwa taifa linakabiliwa na mgawo wa umeme, haina ukweli

Wiki iliyopita, Lipumba akitoa maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF, alisema taifa liko hatarini kukabiliwa na mgawo wa umeme kama Serikali haitachukua hatua za haraka.

Lakini jana, Waziri Muhongo alisisitiza kuwa hakuna mgawo wowote wa umeme, kwa sababu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limejipanga kutafuta vyanzo vingine vya kuzalisha umeme wa uhakika.

Waziri Muhongo, alitoa kauli hiyo mjini Musoma wakati wa kikao kilichoshirikisha vijana wa Manispaa ya Musoma ambao walihoji sababu zinazochangia Mji wa Musoma kukosa maendeleo.

Alisema suala la kukatika kwa umeme dakika mbili ama tatu, si mgawo kama inavyoelezwa na Profesa Lipumba, bali ni kutokana na miundombinu ambayo imechakaa.

Alisema hivi sasa, TANESCO imeelekeza nguvu zake kufanya jitihada za kuibadilisha ili kukabiliana na changamoto hiyo.

"Sote tunafahamu miundombinu ya TANESCO, mingi imechakaa na inahitaji mabadiliko ambayo kwa asilimia kubwa, inafanyiwa kazi…wakati wa matengenezo hupelekea kuwepo na kero ya kukatika umeme kwa muda, lakini si kila siku na huo sio," alisema Waziri Muhongo.

Alisema akiwa waziri mwenye dhamana, atamueleza Waziri Mkuu ama Rais iwapo kutakuwa na mgawo wa umeme, lakini si watu kusimama na kusema kuna mgawo kitu ambacho amekiita ni uzushi ambao unatumiwa na wanasiasa katika propoganda zao, ambazo hazina tija kwa Taifa.

Alisema TANESCO, imejipanga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana na tayari imeanza programu ya kusambaza umeme nchi nzima katika vijiji na wilaya.

Alisema zipo changamoto nyingine ambazo zinafanywa na watu wasio wazalendo kwa kuiba mafuta kwenye transifoma pamoja na waya za umeme.

Akizungumzia masuala ya kimaendeleo katika mji wa Musoma, Waziri Muhongo aliwataka vijana kuacha ubinafsi na badala yake washirikiane kujitafutia maendeleo.

Alisema kukalia siasa kila siku, kamwe mji huo hautabadilika kwa maneno.

CHANZO:MTANZANIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top