Wauguzi.(Picha na Mwananchi)
Kwa ufupi
“Imeniuma sana mwanamke mwenzetu amedhalilishwa
sana, huwezi kuamini amejifungulia korido watu wote wanamwangalia.
Sijapenda hali kama hii inatakiwa ikomeshwe kwani kulikuwa na sababu
gani ya kumfanya nesi wa wodi ya wazazi kushindwa kumsaidia huyu mama,”
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Mama huyo aliyefahamika kwa jina la Tausi Saidi
(29), mkazi wa Mbete katika Manispaa ya Morogoro, alifikishwa
hospitalini hapo na muuguzi wa Zahanati ya Mbete iliyopo Kata ya
Mlimani akiwa ameambatana na ndugu zake Januari 7, saa 10 jioni akiwa
anaumwa uchungu.
Kwa mujibu wa mume wa mwanamke huyo, Kudra
Khalfani alisema kwamba mke wake alianza kupata uchungu na hivyo
kumpeleka Zahanati ya Mbete. Baada ya kufika huko, alilazimika kupelekwa
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro baada ya kuonyesha dalili
za kujifungua.
Alisema baada ya kufika wodi ya wazazi, nesi
waliyeambatana naye aliyemtaja kwa jina moja la Mwacha, aliingia wodini
na kumtaka nesi wa wodi hiyo kwenda kumwangalia mgonjwa wito ambao
alidai haukuitikiwa na muuguzi huyo.
Mwanaume huyo alisema katika hali isiyokuwa ya
kawaida, muuguzi huyo aliwataka kumpeleka mama huyo wodi namba saba ‘B’
bila kutoa msaada wowote ikiwa ni pamoja na kujua hali ya mgonjwa.
“Baada ya nesi kukataa kumpokea mke wangu, kwa
kuwa alikuwa hawezi hata kutembea ilibidi nisaidiwe na watu wanne kisha
tukambeba mikononi, kwa kuwa hata kitanda cha kumbebea hatukupewa, na
kabla ya kufika akasema tumshushe akawa amejifungulia koridoni na mtoto
haikuwa riziki yetu” alisema.
“Imeniuma sana mwanamke mwenzetu amedhalilishwa
sana, huwezi kuamini amejifungulia korido watu wote wanamwangalia.
Sijapenda hali kama hii inatakiwa ikomeshwe kwani kulikuwa na sababu
gani ya kumfanya nesi wa wodi ya wazazi kushindwa kumsaidia huyu mama,”
alisema Mwajuma Ally.
Hata hivyo alisema mimba ya mwanamke huyo ilikuwa
haijafikisha umri wa kujifungua, kwamba alishawahi kupoteza mimba nne na
kwamba ana matatizo katika suala la uzazi.
“Hata mimba hii iliyotoka tayari alishakuwa na
vidokezo vya hatari na aliambiwa asifanye kazi ngumu, lakini inaonekana
alikuwa anafanya kazi ngumu.
Aliongeza kuwa pamoja na kupewa hiyo tahadhari katika kadi yake ya kliniki, ilionyesha kuwa amehudhuria kliniki mara moja tu.
Kuhusu mwili wa kichanga hicho, mganga mkuu huyo alisema ndugu wamegoma kuukabidhi kwa uongozi wa hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari.
Kuhusu mwili wa kichanga hicho, mganga mkuu huyo alisema ndugu wamegoma kuukabidhi kwa uongozi wa hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kidaktari.
Aidha, mmoja wa ndugu zake, Shida Said alipoulizwa
sababu ya kukataa kuukabidhi mwili wa kichanga hicho alisema hakuna
sababu ya kuwapa mwili huo kwa kuwa walishindwa kumsaidia mgonjwa wao.
CHANZO:MWANANCHI
CHANZO:MWANANCHI

Post a Comment