Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MTATIRO:WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA HASEMI UKWELI, ANASIMAMIA UJANJA.


Mradi wa kujenga bomba la kusafirishia gesi MTWARA DSM utalipotezea taifa shs. Trilioni 1 (bilioni 1000) , na fedha hizi zitarudi mikononi mwa mafisadi na baadaye zitakuwa silaha nzito ya wezi hao katika kuhujumu demokrasia na haki za wananchi.

Kuleta GESI kwa bomba DSM ni sawa na ufisadi mwingine wowote ule, wizi ni wizi tu na lazima tuutamke, hata kama wizi huu wa sasa unatetewa na anayejiita "mtoto wa mkulima anayewagharimu wakulima".

Kama suala ni kuwa umeme unapaswa kufikishwa DSM ili kulinufaisha taidlfa zima tujenge mitambo ya umeme Mtwara na tusafirishe umeme wa waya angani ambao ni nafuu na utatumia nusu ya gharama zinazohitajika kutandika bombabla gesi.

Kama hoja ya serikali ni kuileta gesi ya matumizi ya majumbani nchi nzima na kwqmba lazima ifikishwe DSM kuna njia rahisi, bandari ya mtwara imekaa bila kazi yoyote miaka nenda miaka rudi, tunashindwa kuikarabati na kuipanua kwa gharama zisizozidi bilioni 100 kisha tukaanza kusafirisha gesi safi MTWARA hadi DSM kwa njia ya bandari hadi bandari? Nani ameturoga? Nani ametufumba macho tunaoneshwa na hatuoni? Nani ametuziba masikio tunasikilizishwa na hatusikii?

Bomba hili limekuwa bomba, nzi yuko tayari kufia kwenye kidonda. Hawaoni aibu kabisa CCM, hata wizi huu wa wazi wa bomba wanaung'ang'ania kwa nguvu ilimradi tu lengo lao la kupiga "mahela" ya kujipanga na uchaguzi wa 2015.

Watanzania masikini, tunaibiwa hivi hivi na hivi sasa ni kama tuko msibani, vyombo vya habari vimeanza kucheza muziki wa Pinda na kusifia huku vikijua taifa linaliwa na kwamba kuna kila harufu ya rushwa na ufisadi na wizi wa wazi kwenye mradi wa ujenzi wa bomba.....lol...

Yesu wala Mtume Mohhamad hawatashuka kuja kutusaidia katika wizi huu, mungu ametupatia akili na utashi, lazima tuvitumie kudai haki zetu, kupigania maslahi ya nchi yetu, kukataa kuonewa, kukandamizwa na kukubali kutawaliwa bila huruma na "wakoloni weusi".
 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top