Kwa ufupi
ATCL ilisitisha safari zake April 9, 2012 baada ya
ndege yake aina ya Dash 8 kupata ajali katika kiwanja cha Kigoma, hivyo
Shirika hilo kukosa ndege nyingine. Miezi miwili iliyopita shirika hilo
lilinunua ndege mpya
,,,,,,,,
,,,,,,,,
Tukio hilo lilitokea juzi jioni muda mfupi baada
ya ndege hiyo aina ya Bombadia Dash 8 kuruka katika uwanja wa ndege wa
Kigoma, ikiwa katika safari zake za kwanza, baada ya kusitishwa takriban
miezi tisa iliyopita.
ATCL ilisitisha safari zake April 9, 2012 baada ya
ndege yake aina ya Dash 8 kupata ajali katika kiwanja cha Kigoma, hivyo
Shirika hilo kukosa ndege nyingine. Miezi miwili iliyopita shirika hilo
lilinunua ndege mpya.
Kaimu Mkurugenzi wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro
alisema ilipata hitilafu hiyo dakika 15 tangu iliporuka, baada ya kioo
cha mbele kupata ufa.“Ufa ule uliwatisha marubani na waliamua kutua kwa
dharura kwa sababu kioo kingeweza kupasuka na kusababisha ajali mbaya na
ndege kuanguka,” alisema Lazaro na kuongeza;
“Kawaida vioo vya ndege hupashwa moto ndege
inapoondoka na endapo utatokea ufa wowote ni lazima irudi kiwanjani na
kama ipo mbali na kiwanja inambidi rubani ateremke chini na kupunguza
mwendo.”
Alisema kutokana na hali hiyo, wapo kwenye
harakati ya kuifanyia matengenezo ndege hiyo na wakati wowote itarudi
kwenye safari zake za kawaida.
CHANZO:MWANANCHI
CHANZO:MWANANCHI

Post a Comment