 |
| Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) (kushoto) akisalimiana na Mhe. Armando Emillio Guebuza, Rais wa
Msumbiji mara baada ya Rais huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere leo. Mhe. Guebuza ni miongoni mwa Marais
wanaohudhuria Mkutano Maalum wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA)
unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2013. |
 |
| Mhe. Guebuza (kushoto) akifuatana na Waziri Membe mara baada ya kuwasili |
 |
| Mhe. Rais Guebuza wakati alipokuwa akiteremka kwenye ndege mara baada ya kuwasili nchini. |
 |
| Mhe.
Rais Guebuza akiangalia ngoma za utamaduni (hazipo pichani) zilizokuwa
zikitoa burudani kiwanjani hapo mara baada ya kuwasili. |
 |
| Moja ya kikundi cha utamaduni kilichokuwa kikitoa burudani kwa Mhe. Rais Guebuza alipowasili nchini. |
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Thursday, January 10, 2013
Post a Comment