Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

WAZIRI MEMBE ATANGAZA KUTOGOMBEA UBUNGE TENA

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.  
(Picha na mwananchi)
.........
Kwa ufupi
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.
.........................
WAZIRI wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametangaza kuwa hatogomea tena ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Membe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama, mkoani Lindi, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake.
“Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge,” alisema Membe.
, ambapo pia aliwataka wananchi wa mikoa ya kusini, kuwa na subira katika kipindi hiki ambapo Serikali inashughulikia mchakato wa kuvuna gesi asilia.
Alisema kuwa ni muhimu kwa wakazi wa mikoa iliyopatikana gesi kutambua kuwa rasilimali zilinazopatikana nchini ni mali ya Watanzania wote na siyo ya mikoa iliyogundulika pekee.
Waziri Membe aliwataka madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, kuacha kutumia vikao vya halmashauri kujadili malumbano yasiyokuwa na msingi akisema kwamba kufanya hivyo ni kipoteza rasilimali za wananchi bila faida.
“Salamu zangu za mwaka mpya ni kuwaomba madiwani kuacha kutumia vikao kuwajadili madiwani wenzenu kwa hoja zisizokuwa na maana, badala yake tujenge umoja na mshikamano ili kufanya kazi za kusimamia miradi ya maendeleo,” alisema Membe.
Waziri Membe alitumia muda huo pia kuwataka madiwani kujipanga katika kusimamia matumizi ya fedha za miradi ya Halmashauri.
Baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali mikoa ya Lindi na Mtwara walikusanyika jimboni kwa Membe kusherekea kuadhimisha mwaka mpya.
Viongozi walioshiriki katika sherehe hiyo ni pamoja Mbunge wa Mtwara mjini, Hasnain Murji, Godless Kweka ambaye ni Mjumbe wa Nec, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Mkoa wa Lindi ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila na madiwani pamoja na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.
  CHANZO:MWANANCHI  
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top