Wachezaji wa Young Africans wakipasha misuli moto
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Tmu ya Young Africans leo asubuhi imeendelea na mazoezi katika
viwanja vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki
dhidi ya timu ya Denizlispor FC ya ligi daraja la kwanza Uturuki, mchezo
ambao ulishia kwa Denizlispor FC kushinda kwa mabao 2-1, mechi
liofanyika katika uwanja wa Selen football - Kamelya Complex Antalya.
Kocha Brandts ameendelea kukinoa kikosi chake na
kufanyia marekebisho ya baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa
jana ambao hata hivyo Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo
lakini maamuzi ya mwamuzi kipindi cha pili yaliinyima Young Africans
ushindi.
Denizlispor FC timu ambayo imeshuka
kutoka ligi kuu ya uturki mwaka juzi, inapigania kurudi tena katika Ligi
kuuya Uturuki, jana ilishindwa kutamba kabisa mebele ya Young Africans
ambayo iliweza kucheza soka safi na la kuvutia mda wote wa mchezo.
Brandts
amemtupia lawama mwamuzi wa mchezo jana, kwamba maamuzi yake ndio
yalipelekea timu yake kupoteza mchezo huo, kwani vijana wake waliweza
kucheza vizuri kuanzia nafasi ya ulinzi mpaka ushambuliaji hali
iliyowashangaza waturuki hao.
Tazama goli la
kwanza mshambuliaji wao aliunawa mpira kabla ya kufunga na bado mwamuzi
akalikubali bao alilofunga, bao la pili Nadri Cannavaro alichezwa
mazdhambi mshika kibendera akanyanyua kuwa ni faulo lakini cha ajabu
mwamuzi aliamuru ipigwe penati, kiukweli mwamuzi alichangia kutufanya
tupoteze mchezo huo alisema 'Brandts'
Wachezaji
wanaendelea na mazoezi mpaka siku ya jumamosi ambayo itakua ni siku ya
mwisho kabla ya siku ya jumapili kuanza safari ya kurudi nchini Tanzania
tayari kabisa kwa mbio za kuuchukua Uibingwa wa Ligi ya Kuu ya Vodacom
2013.
Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football
Young
Africans imeendelea na mazoezi yake leo asubuhi katika viwanja vya Fame
Residence Football ambapo imekuwa ikifanya mazoezi tangu kuwasili
katika mjii wa Antalya.
Kabange Twite, Haruna Niyonzima & Mbuyu Twite
CHANZO:Young Africans


Post a Comment