Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema akipanda jukwaa la 'walala hoi' Uwanja wa Shikh Amri Abeid mjini Arusha jana kuangalia mechi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,Kati ya Simba na JKT Oljoro.Tofauti na ilivyozoeleka kwa waheshimiwa wabunge kuwa wanakaa jukwaa la VIP Lema alivunja mwiko huo na kujichanganya na machalii hali iliyovutia watu wengi Uwanjani hapo.Mechi hiyo iliishia kwa JKT Oljoro 1-1 Simba.
(Picha na Bongo Stazz Blog)
''Karibu huku mheshimiwa..'' nikila mmoja akiwa na hamu ya kukaa karibu nae wakati alipokuwa anapanda Jukwaani alipojikuta anakaribishwa na kila shabiki akae karibu nae.
''naomba siti,nikae hapa ...'' Mhe.Lema akiomba nafasi ya kukaa huku mashabiki wengine nao wakibaki wakitabasamu kuona Mbunge wao akijichanganya nao.
Post a Comment