Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

UCHAGUZI UDIWANI KATA TANO ARUSHA UTATA

Uchaguzi wa udiwani katika kata tano za Jiji la Arusha zilizo wazi umekuwa na utata kutokana na  Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutoa kauli zinazokinzana.
Wakati Tamiseni ikisema kuwa imeshapeleka taarifa Nec, Tume inasema haijapokea taarifa hiyo na kuwa ikishazipata itawatangazia wananchi.

Akizungumza na NIPASHE juzi mjini Dodoma, Naibu Waziri wa Tamisemi, Kassim Majaliwa, alisema baada ya mahakama kutoa hukumu dhidi ya kesi iliyofunguliwa na madiwani hao ambao walivuliwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walipeleka taarifa Nec.

“Tumeshapeleka taarifa ya viti hivyo kuwa wazi tangu mwaka jana, baada ya rulling (hukumu) ya mahakama na tunachosubiri sasa ni Nec kutoa utaratibu wa uchaguzi na sisi tutapeleka kwa wakurugenzi kwa ajili ya usimamizi,” alisema Majaliwa.


Mkurugenzi wa Nec, Julius Malaba, alisema tume hiyo ikishapata taarifa itatoa taarifa kwa wananchi.

“Lakini ninachosema ni kwamba, kata zote ambazo tume itakuwa imeshaarifiwa ‘immediately’ mara moja tutawatangazia wananchi. Kwa sasa sitataka niingie kwenye ‘specific’ kwa hizi za Arusha pekee, tutakapoambiwa tutaangalia zote zilizopo wazi, tutatangaza kwa wananchi,” alisema Malaba.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameitaka serikali kuitisha haraka uchaguzi wa kata hizo  kabla ya nguvu kubwa ya kushinikiza  uchaguzi huo haijatumika.
Mbowe alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mkoani Arusha.

Alisema inashangaza kuona serikali haitekelezi utawala wa kisheria na kukiuka katiba ya nchi mpaka ishituliwe kwa maandamano.

“Mimi nasema serikali ifanye haraka kuitisha uchaguzi, la sivyo tutalianzisha ‘libeneke’ lisilo na mwisho Arusha kwa sababu haiwezekani wananchi wakose uwakilishi karibu miaka miwili, huu ni uhuni wa wazi,” alisema Mbowe.

Madiwani waliofukuzwa na kata walizokuwa wanaziwakilisha kwenye mabano  ni aliyekuwa Naibu Meya, Estomih Mallah (Kimandolu); John Bayo (Elerai); Reuben Ngowi (Themi); Charles Mpanda (Kaloleni) na Crispin Tarimo (Sekei) pamoja na Rehema Mohamed wa Viti Maalumu.

Walifukuzwa Kamati Kuu ya Chadema baada ya kukaidi maelekezo ya chama hicho kwa kufikia mwafaka na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kumtambua Meya wa Jiji hilo, ambaye ushindi wake ulipingwa na Chadema.

Kwa mujibu wa chama hicho, uamuzi wa kuwafukuza madiwani hao ni kitendo chao cha usaliti.
 
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top