Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA KUIVAA AFRICAN LYON JUMATANO

Kikosi cha Young Africans ambacho kimeingia kambini tangu jana jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya African Lyon siku ya jumatano katika Uwanja wa Taifa , leo asubuhi kimefanya mazoezi katika uwanja wa mabatini kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa keshokutwa.

Young Africans inaongoza msimamo wa ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa na point 33, sawa na timu ya Azam FC yenye point 33, lakini timu ya Yanga ikiwa imecheza michezo 15 na kufunga mabao 29 na kufungwa 12, huku Azam ikiwa imecheza michezo 16 na kufunga mabao 27 na kufungwa mabao 14.

Wachezaji wote wameonekana kuwa wenye  morali ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo zitaifanya timu iendelee kuongoza msimamo wa Ligi Kuu pamoja na kujitengenezea mazingira ya kutwaa Ubingwa.

Kocha Mkuu Ernest Brandts amesema amefurahishwa na nidhamu ya hali ya juu kwa wachezaji wake, kwani wachezaji wote wameweza kufanya mazoezi ya leo, wachezaji watatu walikua nje ya nchi na watano walikua timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) kwa ajili ya michezo ya kirafiki lakni wote wameweza kufanya mazoezi leo. 

Mbuyu Twite ndio mchezaji pekee ambaye hakuweza kufanya mazoezi leo kutokana na kupata majeraha katika mchezo wa kirafiki wa timu yake ya Taifa (Rwanda) dhidi ya timu ya Uganda, hivyo atakua nje kwa siku tatu huku akiendelea kupata matibabu.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top