Yanga kesho inaingia Uwanja wa Taifa kupambana na Kagera Sugar katika mechi ya Ligi kuu katika mechi inayotazamiwa kuwa ya kulipiza kisasi kwa kufungwa na kagera goli 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza.
Yanga inayoongoza Ligi kwa pointi 39 baada ya kucheza mechi 17 ikifuatiwa na Azam Fc 'wana lambalamba' wenye pointi 36 na ikiwa imecheza mechi 18.Wakifuatiwa na Simba wenye Pointi 31 na kucheza mechi 18.
Mechi ya Kesho ni muhimu sana kwa Yanga ambayo inahitaji pointi tatu muhimu ili iweze kujichimbia zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa kuongoza wigo wa pointi 6 kati yake na Azam wanaowafukuzia kwa karibu na kuwaacha kwa mbali Mabingwa watetezi Simba.
Yanga tayari wameingia kambini kujiandaa SOMA[YANGA YAINGIA KAMBINI BAADA YA KUICHAPA AZAM] na mechi kati yake na Kagera Sugar katika hali inaonekana kuwa imedhamiria mwaka huu kurudisha heshima yake kwa kunyakua Ubingwa wa bara kutoka kwa Mtani wake Simba ambaye anaonekana kapoteza muelekeo.
Hivyo Yanga wana kazi kubwa mbili kesho ikiwa ni kusaka pointi tatu muhimu ili kujikita zaidi kileleni huku ikitaka kujifuta machozi kwa kuifunga Kagera Sugar waliowafunga mechi ya kwanza.
Na Chediel
Post a Comment