Hussein Bashe Bashe
---
Ndg
zangu,Awali ya yote niwatakie Juma Pili Njema na Kwa Ndg zetu wanoenda
kanisani siku ya Leo waendelee kuombea Taifa letu na Viongozi wetu
kufanya maamuzi ya Busara juu ya Hatima ya Maisha ya Watanzania na Taifa
kwa Ujumla.
Nimeanza na maneno hiyo hapa juu kufatia matukio miwili,Moja ni
Tukio la Arusha na Pili ni Tukio la Maamuzi ya Baraza la Madiwani la
wilaya ya nzega.
Nzega
Halmashauri ya wilaya
nzega imepitisha Bajeti na mipango ya Mendeleo ya mwaka wa fedha 2013/4
kilichonisikitisha ni Madiwani kujitengea milioni 82 kwa ajili ya ziara
Kwenda mkoa ya Arusha ,Dodoma Kama ziara ya kujifunza,Wakati wilaya
inakabiliwa na Changamoto za uharibifu aw miundo mbinu kufatia muda
Nyingi,makazi ya wananchi wengine yameharibika,shule za msingi na
secondaries hazina Madawati,waalimu hawana nyumba ,vituo vya Afya having
dawa za kutosha,tunakabiliwa na tatiizo la Maji Mijini na vijijini.
Wakati Hali ikiwa hivi fedha hizo ni Intrest(RIBA) iliyotokana na
fedha zilizowekwa benki Baada ya mgodi kutulipa 2bn,Wabunge wakiwa
wajumbe wa kamati ya fedha wamepitisha hili,mbali hapo wameunda tume ya
Watu 15 Kwenda Dar kukutana na Katibu mkuu aw Nishati kufatilia madai
Kila mjumbe atapewa posho ya siku 80,000 kwa siku 10 mbali na posho za
madereva kwani wataondoka na gari za halmashauri,mbali na mafuta,kuna
tume ya kufatilia mji mdogo nayo inawajumbe 10 imetengewa mamilioni ya
pesa.
Mbali na Hilo wakubwa wameamua kumchukua fedha 2bn kuanzisha Benki
ya Maendeleo ya Nzega ikiwa na dhamira ya kutoa mikopo kwa Wananchi aw
Nzega,wanafanya maamuzi haya huku wakifahamu Halmshauri ya wilaya ya
Nzega Ina Fedha za Mfuko aw Maendeleo ya Vijana ,Mfuko aw Maendeleo ya
Kina Mama ,Mabilioni ya Jk vyote hivi vimeshindwa kusimamiwa na Fedha
zake kwa Miaka yote hazijawahi kuwa na Mrejesho chanya Leo tena
wanatenga fedha ili kuanzisha Benki itakayoendeshwa na Watu wale
wale,kwa Mfumo ule ule,kuwakopesha Watu wale wale ambao Mara zote
wanaposhindwa kurejesha hutumika sasa zile zile kuwasamehe.
Huu ni mchezo kwenye maisha ya wananchi aw wilaya ya nzega ambao hawana
High school ,hawana barabara za uhakika,waalimu hawana makazi,wanafunzi
hawana maabara,hawana Madawati,zahanati hazina Madawa,mikopo ya
Mabilioni ya Jk haikufanikiwa,mikopo ya Mfuko aw Maendeleo wa Vijana
haikufanikiwa,mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Kina mama haikufanikiwa
Leo zinatengwa fedha za kuanzisha Benki ya kukopesha wana nzega,kuna
Mabenki mawili nzega,kuna taasisi za mikopo zaidi 5 kwa matatizo
yanayokabili wilaya lie huu ni Kupoteza fedha za wananchi wa nzg kwa
posho na kuandaa maradi ambayo haina Tija.
TUKIO LA ARUSHA.
Tukio la kuuwawa Kijana aw Chou cha uhasibu na
matokeo Yake badala ya kutafuta wauwaji kunatengenezwa mazingira ya
kuleta Instabillity kwa kumkamata LEMA, Kaka yangu Mulongo katika hili
alivolisimamia na kulitekeleza ameonyesha Udhaifu aw Hali ya Juu na
matokeo Yake inavunjia heshima Serekali ya Chama chetu na Kuongeza chuki
dhidi ya CCM Hakukua na sababu ya Kubahave the way he did pale
chuoni,alionyesha kiburi hakua humble,hakutumia Busara katika jambo
hili.
Wakati kuna Kijana ameuwawa,na yeye ndie Rais wa eneo lile attitude
alionyesha Hakukua na leadership pale,tunakabiliwa na uchaguzi kuna mtu
ameuwawa na si Tukio la kwanza,Nguvu iliyotumika kumkamata lema Leo CCM
mkoa aw Arusha wanakabiliana na maswali mengi kuliko Majibu,inasikitisha
viongozi wanaotuwakilisha kuongoza ndio hao tunawaona Bungeni,ndio hao
Kina Mulongo na maamuzi na attitude ya kaka Mulongo,ndio hao Kama Baraza
la Madiwani aw Nzega ambao kwao semina safari,posho,maradi
isiyotekelezeka,kuunda tume ya kuchunguza madai ya wafanyakazi ni
kuitengea fungu Wakati kk Bajeti wameisha tenga fedha za kulipa madeni
halafu unaunda tume ya kuchunguza madeni ambayo umeisha lipa.
Ndg zangu wana CCM chuki za Watanzania dhidi ya chama chetu
zinaongezeka Kila siku na hii ni kutokana na Tabia zetu wenyewe Wakati
hospitalini hakuna Vifaa vya Kina mama kujifungulia sisi tunajitengea
fedha za ziara 82m,posho za 80,000 kwa siku,tunaanzisha miradi ambayo
haitawasaidia wananchi kk kero zao za Kila siku,Wakati mwanafunzi
ameuwawa na kibaka tunatumia mabomu,Rundo la Askari kumkamata mtu Moja
kwakua si mwana CCM,wananchi nyumba zimebomolewa na mvua,hakuna Bajeti
ya kuwasaidia hawa Watu,hakuna Madawati,dawa hospitali,tunaelekeza fedha
ktk mambo yasiyogusa maisha Yao.
Unless tubadilike na kuanza kutambua Watanzania hawajatupa madaraka
ilituchezee maisha Yao,unless tutambue uongozi ni dhamana tutendelea
kuchukiwa na Leo sitashangaa Arusha tukipoteza kata 4 zilizowazi,tunawalazimisha Watanzania kutafuta matumaini kwa wapinzani
kwa sisi wenyewe kuamua kujipa Utawala badala ya Uongozi.Binafsi swala
la nzega nimekiandikia Barua chama changu wilayan kukiomba kutazama upya
maamuzi ya Full Council na kutambua upya vipaumbele halmashauri ya nzg
inakabiliwa na Changamoto Nyingi hawatakiwi kuchezea fedha za walipa
kodi.Hili la Arusha CCM inatakiwa kutolishabikia RC amemishandle the
whole thing.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Monday, April 29, 2013
Post a Comment