Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige wakiwakikabidhi
zawadi mbalimbali kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Matumaini cha mjini Dodoma.
--
Asasi ya Kijamii ya Catherine Foundation jana
imetembelea kituo cha kulelea wa watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani
Dodoma ambapo walikwenda kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa
Asasi hiyo, Catherine Magige.
Katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa
Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo,
Madaftari, Mafuta, Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za
watoto, kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia
katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine
Magige akihutubia katika hafla hiyo jana.
Post a Comment