Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

POLISI:KUNA DALILI ZA KUIBUKA AL QAEDA, AL SHABAB NCHINI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Said Mwema.
Jeshi la Polisi nchini, limesema zipo dalili za kuibuka makundi ya kigaidi ndani ya nchi yakiratibiwa na makundi ya Al Qaeda na Al Shabab.
Kwa msingi huo, jeshi hilo limewataka viongozi wa kisiasa kuchukua hatua ya kuwatahadharisha wananchi kuhusu vitendo vya uvunjifu wa amani kwa maendeleo ya kitaifa ikiwemo sekta ya utalii.

Tahadhari hiyo ilitolewa na Kamishna Mwandamizi wa Polisi Hussein Nassor Laisseri, alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hali ya uhalifu Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar katika semina ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Semina hiyo iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, ilijadili mpango kazi wa kuboresha Jeshi la Polisi nchini.

“Taarifa za kiintelijensia zinatutahadharisha kuhusu uwapo wa magenge ya kigaidi Al Qaeda na Al Shabab nchini mwetu pamoja na kuibuka makundi ya kigaidi ya ndani,” alisema SACP Laisseri.

Alisema matukio yaliyotokea nchini Kenya na Uganda, yamezalisha uwapo wa mtandao wa magenge ya ugaidi nchini kwa vile miongoni mwa waliopanga na kusaidia ugaidi huo, walitoka Tanzania.

Hata hivyo, alisema Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wana jukumu kubwa la kuwaelimisha wananchi kuhusu mbinu za uhalifu mpya pamoja na madhara ya matishio ya amani nchini ili kuwaepusha kupata hasara au madhara yanayotokana na uhalifu au vitendo vya vurugu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, alisema maboresho yanayofanywa ndani ya jeshi hilo, ndiyo njia pekee itakayosaidia kupambana na uhalifu na kuwataka viongozi kuunga mkono hatua zinazoendelea kuchukuliwa.

Alisema uongozi wa jeshi hilo umepokea maoni ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kazi yao kubwa ni kuyafanyia kazi ili kuhakikisha hali ya amani inaendelea kudumishwa Tanzania Bara na Zanzibar.
 
CHANZO: NIPASHE
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top