Baadhi nya madhara ya utumiaji wa vipodozi vyeme kemikali  
............. 
Kwa ufupi
            Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha 
Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia, 
kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo’ Tanzania umebainisha hayo
Wanawake zaidi ya 6milioni nchini huenda wakaugua saratani, 
kuzaa watoto wenye mtindo wa ubongo au kupoteza maisha kutokana na 
kukithiri kwa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali hatari.
Utafiti wa Profesa Msaidizi wa Chuo Kikuu cha 
Georgia, Atlanta, Marekani, Kelly Lewis wa kitengo cha Sosholojia, 
kuhusu wanawake wanaotumia ‘mkorogo’ Tanzania umebainisha hayo.
                
Taarifa ya utafiti huo inaonyesha kuwa asilimia 30
 ya wanawake, sawa na 6 milioni ya wanawake wote nchini ambao ni milioni
 23, wanatumia vipodozi vyenye kemikali hatari, vyenye madini ya zebaki,
 hydroquinone na maji ya betri.
                
Dk Lewis akishirikiana na timu ya Watanzania 20, 
aliwahoji wanawake 420 katika Jiji la Dar es Salaam ambapo wengi 
walikiri kujichubua kwa sababu ya dhana kuwa weupe ni uzuri, pamoja na 
kuwaridhisha wenza wao wanaopenda wanawake weupe.
                
Utafiti huo wa Shahada ya Uzamivu ulifanyika kuanzia mwaka 2000 na kumalizika Mei 17, 2012.
                
Profesa Lewis anasema kuwa vipodozi hivyo hasa 
vyenye madini ya zebaki, kwa kiasi kikubwa husababisha ugumba, saratani 
na maradhi ya figo.
“Inatisha.
                
              “Inatisha.
Wanawake hawatumii ‘mikorogo’ ya dukani pekee, 
lakini pia wanatengeneza mikorogo ya kijadi kwa kuchanganya asidi ya 
maji ya betri ya gari, dawa ya meno na sabuni ya unga,” anasema Dk 
Kelly.Akizungumza kwa njia ya Barua Pepe, Profesa Lewis anasema kuwa 
anatarajia kufanya kipindi kuhusu wanawake wanaotumia mikorogo Tanzania 
ili kutoa elimu.
                
‘Kutokana na maombi mengi, nimefungua Kituo cha Utalii kwa Umma na nitafanya safari mbili za kuja nchini Tanzania,” anasema.
                
TFDA imebainisha vipodozi vyenye sumu kuwa ni 
pamoja na ni Carolight, inayotajwa kuwa na sumu kali zaidi pamoja na 
vile vyenye madini ya zebaki au mercury, ikiwamo sabuni ya Jaribu na 
Mekako.
                
Vipodozi vingine ni vile vilivyochanganywa na 
viambata sumu kama Clobetasol na Betamethasone ambapo itajwa pia krimu 
ya Amira, Betasol na Skin Success.
                
Inaelezwa kuwa wanawake wanaotumia mafuta ya aina hiyo wakiwa wajawazito huwaathiri watoto walioko tumboni.
                
Asilimia 70 ya vipodozi hivyo hutoka nje ya nchi, ambapo imebainika kuwa hakuna sheria kali za udhibiti wa dawa na vipodozi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa asilimia 10 ya dawa duniani kote ni bandia au duni.
Taarifa zaidi zinasema kuwa zaidi ya asilimia 50 
ya dawa bandia zinatengenezwa kutoka katika maabara za chini ya ardhi 
zilizopo China na India.
Dawa bandia ni zile ambazo mtengenezaji amebadili 
viambata, nembo, vifungashio au amedanganya kwa namna yeyote kwa lengo 
la kujipatia kipato.
Dawa duni ni zile ambazo mchanganyiko wa viambata vyake haukidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kisayansi.
Dawa duni ni zile ambazo mchanganyiko wa viambata vyake haukidhi viwango vya ubora vinavyokubalika kisayansi.
Dawa bandia zilizokamatwa na TFDA
Mkurugenzi wa Shirika la Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Paul Sonda, anasema kuwa Agosti 2011 dawa ya Malaria aina ya Laefin, ilitengenezwa na kusambazwa katika mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora, Shinyanga na Kagera.

Dawa hiyo ilighushiwa kwa teknolojia ya hali ya 
juu.Watengenezaji hao waliweza kunakili kila kitu kasoro herufi moja 
katika jina, ambapo badala ya kuandika Laefin waliandika ‘Laifin’ wDawa 
nyingine ya Malaria, aina ya Coartem ilitengenezwa na kusambazwa 
madukani na dawa halisi ilitakiwa kutumika kuanzia Machi, 2007 na kwisha
 muda wake Februari 2009.
“Baada ya kwisha muda wake, wajanja walibadili 
muda na kuandika imetengenezwa Machi 2009 na muda wake utakwisha 
Februari, 2012,” anasema.
Dawa hiyo ilisambazwa zaidi katika Wilaya za Kilombero na Ulanga Morogoro kuanzia Agosti na Septemba 2011.
Ibrufen
Sonda anasema kuwa dawa ya maumivu ya Ibuprofen iliuzwa kama Erythromycin (antibiotic inayotibu magonjwa ya kuambukiza)
Kwa kuwa Ibuprofen na Erythromycin zinafanana kwa rangi na kwa umbo, wajanja walitumia mfanano huo na kuziweka katika mfumo wa soko.

Dawa hizo zilipatikana katika mikoa ya Ruvuma katika Hospitali ya Litembo
Wilaya ya Mbinga
Eloquine
Sonda anaongeza kuwa pia mwezi Februari mwaka 2011, dawa ya malaria aina ya Eloquine au Kwinini Sulphate ilighushiwa na iligundulika katika maeneo ya Moshi, Kilombero na Ulanga.
Eloquine
Sonda anaongeza kuwa pia mwezi Februari mwaka 2011, dawa ya malaria aina ya Eloquine au Kwinini Sulphate ilighushiwa na iligundulika katika maeneo ya Moshi, Kilombero na Ulanga.
Sonda anasema kuwa TFDA ilibaini kuwa vidonge vya 
Eloquine havikuwa na kiambata cha ‘Quinine Sulphate’ badala yake 
uchunguzi ulibaini kuwa ni dawa ya kuzuia kuharisha aina ya Flagyl au 
Metronidazole.
Dawa aina ya Pen V, ilitengenezwa na kile kinachodaiwa kuwa ni unga wa ngano.
Pen V hutumika kutibu maradhi ya kuambukiza, vidonda. 
(Antibiotic) Wakaguzi walipoikagua waligundua kuwa dawa hiyo inaganda 
ndani ya kopo pindi unapoliinamisha.
Bidhaa zinazosadikiwa kukuza maumbile(hip lift up 
na hip massage cream), nazo zilipigwa marufuku ingawa bado zinauzwa kwa 
njia ya panya katika maduka.
Mkurugenzi huyo wa TFDA Kanda ya Nyanda za Juu 
Kusini anasema kuwa thamani ya dawa, chakula na vipodozi 
vilivyoteketezwa na mamlaka yake kwa mwaka 2010/2011 ni Sh844. 3 
bilioni.
Madhara
Sonda anasema kuwa matumizi ya vipodozi vyenye viambata sumu kwa kaisi kikubwa husababisha maradhi ya figo, fangasi, saratani ya ngozi, ini na mzio.
Mfamasia katika Hospitali ya Amana, Christopher Masika anasema kuwa Serikali pamoja na wadau wengine wa afya hawana budi kuwafundisha Watanzania namna ya kubaini dawa bandia.

Anasema kwamba matumizi ya dawa bandia yana 
madhara mengi. “Kwa mfano Flagyl haitibu malaria bali inatibu vimelea 
vya maradhi ya tumbo, mtu akinywa kwa lengo la kutibu malaria atakuwa 
hajatibiwa na ugonjwa wake utakuwa palepale na baada ya siku chache 
malaria inaweza kujirudia,” anasema.
Anasema kuwa ndiyo maana siku hizi dawa za malaria
 zinakuwa sugu na watu wanaendelea kuugua ugonjwa huo kutokana na ujanja
 mbaya unaofanyika.Kuhusu vipodozi vyenye viambata sumu, Famasia Masika 
alisema kuwa vipodozi vyenye madini ya Zebaki au Mercury husababisha 
maradhi ya saratani.
“Kwa mfano hydroquinoline, hiki ni kiambata sumu 
ambacho kinaharibu ngozi, ni rahisi kupata maambukizi ya ngozi kwa 
sababu ngozi ya mtumiaji inakuwa nyepesi mno.
Mtu huyo si rahisi kupona hata akijeruhiwa,” anasema
Anasema ngozi ya binadamu ina kinga iitwayo ‘therapine’ ambayo hupukutishwa mtu anapotumia vipodozi vyenye viambata sumu.
Hivyo ni rahisi kupata saratani kwa kuwa kinga hiyo huondolewa.
Anasema ngozi ya binadamu ina kinga iitwayo ‘therapine’ ambayo hupukutishwa mtu anapotumia vipodozi vyenye viambata sumu.
Hivyo ni rahisi kupata saratani kwa kuwa kinga hiyo huondolewa.
“Lakini pia matundu ya kutolea uchafu yanazibwa, hivyo mwili hautoi uchafu na sumu inabaki mwilini,” anasema Mfamasia Masika
Anasema kuwa mwanamke anayetumia vipodozi hivyo, ngozi yake huwa laini mno na chochote kitakachoingia huiathiri.
Anasema kuwa mwanamke anayetumia vipodozi hivyo, ngozi yake huwa laini mno na chochote kitakachoingia huiathiri.
Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza anasema
 kuwa mamlaka hiyo imepiga marufuku vipodozi vyote vyenye viambata sumu,
 ingawa bado watu wanavitumia.“Madhara yake ni makubwa, mwanamke 
mjamzito ni rahisi kuzaa mtoto taahira, au mimba ikatoka,” anasema 
Simwanza.
Daktari wa Magonjwa ya Ngozi wa Kituo cha Afya 
Centre, Isaack Maro, anasema wanawake wanaotumia vipodozi vyenye 
viambata sumu huathirika kwa kiasi kikubwa bila kujijua.Anasema madini 
ya zebaki yanayotumika katika vipodozi vingi hayatoki kwa urahisi 
mwilini.
Dk Maro anasema madini hayo hujazana mwilini kwa muda mrefu na kusababisha maradhi.
“Watu wanaotumia vipodozi hivyo figo zao huwa zimetoboka kutokana na kuharibiwa na madini ya zebaki” anasema
Pamoja na madhara hayo, wanawake wanaotumia mikorogo ni asilimia 30 Afrika Mashariki.
Pamoja na madhara hayo, wanawake wanaotumia mikorogo ni asilimia 30 Afrika Mashariki.
Jinsi ya kuigundua dawa bandia
Kwa kawaida kuibaini dawa bandia ni lazima uwe umepitia utafiti wa kimaabara. Hata hivyo, zipo njia za awali za kubaini dawa bandia.
*Hukatika kwa urahisi au kupata ufa
*Ina harufu ya ajabu, ladha au rangi
*Wakati mwingine watengenezaji wa dawa bandia hukosea tarakimu, kufunga, vifungashio
*Huuzwa kwa bei rahisi ukilinganisha na dawa halali.
NA MWANANCHI

Post a Comment