Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

NYONGEZA ZA MISHAHARA ZIWIANE NA PATO -WASOMI

 Baadhi ya wafanyakazi wa Manispaa ya Dodoma wakifurahia wakati wa kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Mjini Dodoma . 
Picha na Edwin Mjwahuzi  
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Dar es Salaam.Baadhi ya wasomi nchini wametaka kupanda kwa mishahara kuendane na ongezeko la pato la taifa ili kuepusha mfumuko wa bei katika nyanja mbalimbali.
Kauli ya wasomi imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi.
Alifanya hivyo wakati akiwahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya.
Rais Kikwete alisema nyongeza ya mishahara ya sekta binafsi itatangazwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka atakaposoma bungeni, makadirio na matumizi ya bajeti ya wizara yake katika mwaka wa fedha wa 2013/14.
Rais Kikwete alisema kuwa, wafanyakazi wa sekta ya umma wataongezewa mishahara baada ya kusomwa kwa bajeti kuu.
Wakizungumza kwa nyakati na mahali tofauti jijini Dar es Saalam jana, wasomi na wachumi hao walisema kuwa, ikiwa Serikali itaongeza makusanyo ya kodi, ongezeko la mishahara halitawaathiri wafanyakazi, jambo ambalo linaweza kuwapunguzia makali ya maisha.
“Rais Kikwete anapaswa kutambua kuwa, hata mkulima anahitaji pato zuri, lakini pia kuna baadhi ya wafanyakazi hawana mishahara rasmi, nao pia wanahitaji pato zuri. Ikiwa Serikali itafanikiwa, itaweza kuwasaidia Watanzania kwa jumla,”alisema Profesa Delphin Rwegasira ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alisema, Serikali inapaswa kuzingatia kuwa ukuaji wa pato la taifa, unawagusa Watanzania wote bila ya kuangalia matabaka.
Dk Honest Ngowi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, alisema hali ya uchumi miongoni mwa Watanzania wengi si nzuri.
Dk Hajji Semboja alisema Serikali inapaswa kupanga bajeti ya nyongeza ya mishahara ili itakapopitishwa, wafanyakazi waweze kuingiziwa kwenye mishahara na si kuzungumza kisiasa.
“Kama Rais ametangaza neema ya mishahara, Serikali inapaswa kuingiza kwenye bajeti yake mapema,” alisema.

NA MWANANCHI
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top