KOCHA wa Manchester United, David Moyes
amepata pigo lingine baada ya kiungo wa Barcelona, Cesc Fabregas
kumuambia kocha wake, Tito Vilanova anataka kubaki kwa vigogo hao wa
Katalunya ili kuweza kupata mataji zaidi.
United ilithibitisha kutenga dau la Pauni Milioni 26 kwa ajili ya Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal ili kuweza kuungana na RVP ambao waliwahi kucheza pamoja.
Harakati hizo zilikuja baada ya Thiago
Alcantara kuamua kujiunga na kocha wake wa zamani, Pep Guardiola katika
klabu ya Bayern Munich badala ya mabingwa hao wa England.
Na sasa kocha wa Barca, Vilanova ameanza mazungumzo na Fabregas ambaye ameweka wazi anataka kubaki Nou Camp.
Vilanova alisema: "Cesc amepata ofa
kutoka klabu nyingine. Nimezungumza naye na ameniambia anataka kubaki.
Ndoto zake ni kung'ara akiwa hapa ''
Post a Comment