Edinson Cavani akiwa ameshikilia jezi ya PSG baada ya kusaini kwa Pauni Milioni 55kuichezea klabu hiyo.
Cavani(kushoto) na Mwenyekiti wa PSG, Nasser Al-Khelaifi wa Qatar wakati akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari hiyo jana baada ya kusaini kuichezea klabu ya PSG.
....
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka
26 anayesajiliwa kwa bei mbaya zaidi majira haya ya joto, anaungana na
wachezaji wengine bora waliosajiliwa awali na timu hiyo, Zlatan
Ibrahimovic, Marco Verratti, Ezequiel Lavezzi, Lucas Moura, Javier
Pastore na Thiago Silva.
Cavani anatarajiwa kutengeneza pacha
kali ya ushambuliaji kwa pamoja na Ibrahimovic, ambaye alishinda tuzo ya
Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligue 1 baada ya kufunga mabao 30 msimu
uliopita.
Kocha mpya wa PSG, Laurent Blanc pia
atatumai Cavani na mchezeshaji Lavezzi wataendeleza ushirkkiano wao
mzuri waliokuwa nao Napoli.
Post a Comment