Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria
Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwete amesema kuwa walichelewa kufanya
mawasiliano na vyombo vinavyohusika ili kupata fursa ya kumkabidhi Rais
wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kama walivyokuwa
wamepanga.
Profesa Mbwete akizungumza kwa njia ya simu
alisema kuwa, ingawa Rais Obama ameondoka nchini bado wana njia mbili za
kuweza kumkabidhi cheti ikiwa ni ishara ya kumtunuku shahada hiyo.
“Yule ni mtu mkubwa bwana ingetakiwa tufanye
mawasiliano ya kupata nafasi kumkabidhi kwa miezi mitatu kabla, hata
hivyo hiyo shahada kwa maana halisi tulishampa kwa sababu mkuu wa chuo
ndiye mwenye mamlaka ya kuitoa, kilichokuwa kikisubiriwa ni kumkabidhi
cheti tu na yeye atoe hotuba ya kuikubali,” alisema Profesa Mbwete.
Anasema kuwa, chuo hicho kitawasiliana na Ubalozi wa Marekani nchini ili kuona njia itakayotumiwa katika kumalizia mchakato huo.
“Kwa sasa kuna njia mbili za kumabidhi, sisi
tunaweza kwenda ama tunaweza kukituma cheti hicho kupitia ubalozi na
yeye akatuma hotuba yake,” alisema Profesa Mbwete.
CHANZO:MWANANCHI
CHANZO:MWANANCHI

Post a Comment