|
|
WATANZANIA wametakiwa kuepuka matumizi ya ndoo zinazohifadhiwa
rangi kwa ajili ya kuhifadhia maji ya kunywa kutokana na ndoo hizo kuwa
na athari kiafya.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam,
Mhadhiri Mshauri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi cha Muhimbili
(MUHAS), Dk. Vera Ngowi, alisema kuwa ukosefu wa elimu ya athari ya
viuatilifu imekuwa chanzo cha jamii kushindwa kubaini athari zinazoweza
kuwapata.
Dk. Ngowi alisema ndoo hizo si salama kwa matumizi kutokana na rangi
kuwa na kemikali zinazoweza kusababisha magonjwa mbalimbali ikiwamo
saratani.
Alisema ni muhimu viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo vikaweka
tahadhari ili jamii iepuke kutumia ndoo hizo kwa ajili ya kuhifadhia
maji.
“Hivi sasa baadhi ya Watanzania wanapenda kutumia ndoo hizo kwa ajili
ya kuhifadhia maji, lakini napenda kuwaasa waepuke matumizi ya vifaa
hivyo kwa kuwa vinaweza kusababisha magonjwa ya ngozi na hata saratani,”
alisema.
Alisema watengenezaji wa bidhaa mbalimbali walio wengi wanashindwa
kusema ukweli kuhusiana na madhara yanayoweza kupatikana kwa kuwa
wanahofia kupata hasara.
CHANZO:Tanzania Daima
|
|
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
Jamii
on Tuesday, July 16, 2013
Post a Comment