Kupata makala zaidi za IT, like kurasa yetu: https://www.facebook.com/dudumizi
Kama wewe ni mfanyabiashara wa kati au juu, basi kuwa na Website ni
moja ya vitu vya lazima kwa dunia ya sasa. Takwimu zinaonesha, kuna
Watanzania milioni tano wapo online kila siku. Hapa hawajajumlishwa wale
walio nje ya nchi.
Kuwa na Website ya kampuni kunafungua milango zaidi kwa biashara
yako, kila kona ya dunia inayofikika kwa intaneti, basi website yako
inaweza kufika. Kwa kutumia mitambo ya utafutaji (searh engines) kama
Google, Yahoo, Bing nk, watu ni
rahisi sana kutafuta wanachokitaka online. Hivyo usipoteze nafasi hii ya kipekee kabisa.
rahisi sana kutafuta wanachokitaka online. Hivyo usipoteze nafasi hii ya kipekee kabisa.
Katika makala za awali, tumeandika sana umuhimu wa website, mambo ya
kuzingatia nk, leo hii tutaangalia hatua muhimu za kupitia hadi kumiliki
website. Hivyo twende kazi...
1.Andaa bajeti
Bajeti ni kitu cha awali kama unataka kabisa kwenye kuendea kuwa na
website. Siku hizi teknolojia imerahisishwa, unaweza kuwa na website
inayoendana na bajeti yako. Siyo lazima uwe na mamilioni ili uwe na
website, hakikisha unajieleza ipasavyo pindi unapowasiliana na
watengeneza website ili kuwafahamisha ukomo wa bajeti yako na wao
wataweza kukupa website iliyo ndani ya kikomo chako.
Kwa mfano, kuhost website ya kawaida haizidi elfu 60 za Kitanzania
kwa mwaka,na kutengeneza website ya kawaida pia huanzia laki tatu za
Kitanzania kwa kampuni ya kawaida,ingawa wapo wanaochaji chini au zaidi
ya hapo. Kwa wamiliki wa makampuni makubwa kama Facebook au Google
yanatumia mabilioni kuhakikisha website zao zinakuwa hewani bila tatizo.
Hivyo, bajeti haziwezi kuwa sawa, usiogope kujadiliana na mtengeneza
Website yako, kama ukipata kampuni iliyo makini, watakusaidia kufikia
malengo.
2. Andaa vitu unavyotaka au website unazozipenda
Website ni sehemu ya kampuni, mara nyingi watu huanzisha kampuni
baada ya kuwa na wazo fulani, wazo hili ama linaweza kuwa limetoka kwao
moja kwa moja ama ni baada ya kuangalia toka kwa wengine. Hivyo, katika
hatua hii, andaa vitu unavyotaka viwemo kwenye website yako pia na
orodha ya websites ambazo unapenda vitu fulanifulani toka huko.
Kwa kampuni ya kawaida, unahitaji vitu kama kuhusu sisi, huduma
tunazotoa, wasiliana nasi pia fomu ya mawasiliano ambapo mtu anaweza
kukutumia maobi ya huduma moja kwa moja online.
3 Tengeneza Website
Katika hatua hii, ambayo nayo ina viji hatua kibao ndani yake,
utatengeneza website, ama kwa kutumia timu yako au kwa kuajiri kampuni
nyingine. Siku hizi Tanzania kuna makampuni mengi sana yanayojihusisha
na utengenezaji wa website, unaweza kugoogle na kuyapata. Dudumizi.com ni chagua murua juu ya hili.
Pia, unaweza kutumia programu nyingi za bure zinazopatikana online
kutengeneza website kama Wix.com. Kitu cha muhimu kwenye hili, hakikisha
unatengenezewa Website yenye kukuwezesha kubadili na kuichunga website
bila kuwa na utaalamu wowote. Siku hizi kuna programu (CMS) nyingi kama
Joomla, Wordpress, Drupal nk ambazo zitakusaidia kwenye hili. Bajeti ya
website ya kawaida hucheza laki tatu hadi tano. Kumbuka, sio kila
king'arachi ni dhahabu, kuna kamampuni mengi yanayosema watakutengenezea
website kwa gharama ya chini, ila siku ya mwisho unajikuta unaishia
kujuta.
Kama utaamua kuajiri kampuni, hakikisha umepitia kazi zao walizofanya
na kuridhika na ubora wa kazi zao. Pia kama utaweza hakikisha
unawasiliana na wateja wao kujua ubora wa huduma zao baada ya kazi
kuisha. Kwenye hili, kitu cha muhimu kuzingatia pia, ni juu ya uchungaji
na uboreshaji wa website, kwani kuna kipindi website italeta matatizo,
je nani ni muhusika?
Kama wewe ni mmiliki wa biashara ndogo, hakuna haja ya kuajiri mtu wa
IT kwa ajili ya hili, hivyo unaweza kuwapa jukumu hili watengenezaji wa
website wakusaidie kuichunga website yako na wewe ukaendelea na mambo
mengine ya biashara. Ila, kumbuka kutaka taarifa za maendeleo ya website
yako (web analytics).
4.Chagua jina bora la website
Hii
ni moja ya sehemu inayowachanganya wengi mno, wengi wamekuwa
wakichanganya na kudhani kwamba jina la website ni lazima liendani na
jina la kampuni.Hii siyo lazima, jina la website linaweza kuwa tofauti
kabisa na lile la kampuni, ingawa kama litakuwa sawa bila kuleta
mkanganyiko ni bora zaidi.Ukweli ni kwamba, majina mazuri mengi tayari
yameshachukuliwa, hivyo kuna wakati kama nataka jina la website liendane
na la kampuni yako, basi itakuwia ugumu na kukulazimisha kuongeza
majina ya ziada ili kulifanya liwe la kipekee.
Jina la website ni roho ya website, kwani ni jina ambalo litasambaa
kwenye mitandao na watu wote kulifahamu. Hakikisha jina lako lipo la
kipekee, epuka kutumia majina ya website ambayo yana maneno mengi, yenye
kuchanganya lugha mbili tofauti,
yenye maneno yanayofanana; mfano to, two, 2, II nk. Jina la website
lazima liwe linalotamkika kwenye simu na pia lisilo na miambatano mingi.
Chukulia mfano, Dudumizi.com, linatamkika kiurahisi karibu toka kwa
watu wa sehemu zote Duniani.
Mambo mengine ya kuzingatia hapa ni kuepuka kununua jina la Website
toka kwa makampuni ya uchochoroni, kwani jina lako ni ruru yako kama hii
kampuni itakufa katikati ya safari basi unajiweka kwenye hatihati. Pia,
hakikisha jina linasajiliwa kwa kutumia taarifa zako na si za kampuni
iliyokusajilia.
Mwisho kabisa, msisitizo ni kuwa, jina la Website siyo lazima liwe
jina la kampuni, mfano jina la kampuni yetu ni Dudumizi Technologies,
ila tunatumia jina la Dudumizi kwenye website kwani tungetumia
Dudumizitechnologies.com lingechanganya watu kwakuwa ni refu na
limechanganya lugha mbili hivyo kuleta utata kutamkika, pia kuna watu
wangeliita Dudumizitechnology.com nk.
Gharama za kununua jina la Website ni shilingi elfu 20 kwa .com,
.net elfu 24 kwa .org wakati ile ya .co.tz inaanzia shilingi elfu 25.
5. Chagua wapi pa kuweka Website (Hosting)
Baada ya kuchagua jina, na kununua, ingawa wengi hupenda kufanya
hatua ya nne na ya tatu pamoja, kinachofuata ni kuchagua mahala ambapo
website yako itakaa (Hosting).Siku hizi , gharama za kuhost website
zimeshuka sana, kulingana na Dudumizi Hosting gharama ya kuhost website haizidi elfu 60 kwa website ya kawaida, hii ikijumuisha email ya kampuni.
Kwenye kuchagua wapi pa kuweka website yako, kama ilivyo kwenye jina,
hakikisha unachagua kampuni inayoeleweka. Hakikisha umetembelea website
yao na kuona baadhi ya website zinazohostiwa huko. Tembelea hizi
website kabla ya kuamua. Mambo ya kuzingatia hapa ni kama;
-Muda ambao website itakuwa online bila kupata tatizo (Reliability);
Ukweli ni kuwa, haiwezekani mitambi ikaka mwaka mzima bila kuleta
hitilafu hata siku moja, hivyo hakikisha hizi hitilafu sio nyingi,
-Muda wanaotumia kutatua hitilafu (Maintainability); hakikisha, wanatatua tatizo haraka iwezekanavyo kunapotokea hitilafu na huduma kurudi kwenye mstari.
Vitu hivi, unaweza kuvipata kwa kuwasiliana na wamiliki wa website
zilizohostiwa kwao au kwenye mkataba wa makubaliana ya huduma (SLA).
Hadi hapo utakuwa tayari una website inayofanya kazi, na sasa unaweza kuiweka kwenye kadi na matangazo ya biashara yako na kuwaambia wateja.