Hatumwi mtoto Dukani:
Hiyo ndo kauli iliyotawala vinywani mwa wapenzi, washabiki na wadau wa
soka kuelekea mchezo wa kesho Nani Mtani Jembe dhidi ya Vinara wa Ligi
Kuu ya Vodacom Yanga SC watakapombana na Simba SC katika dimba la uwanja
wa Taifa kesho jumamosi kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za
Afrika Mashariki.
Mchezo huo wa kirafiki ambao
umeandaliwa na wadhamini wa vilabu vyote viwili kupitia kampuni ya bia
ya TBL na kinywaji chake cha Kilimanjaro Premier Lager unatazamiwa kuwa
na washabiki wengi kutokana na kuvuta hisia za wapenzi wa soka.
Young
Africans SC itaingia uwanjani ikiwa na kikosi kamili kilichokamlika
kila idara kufuatia wachezaji waliongezwa kipindi cha dirisha dogo Juma
Kaseja, Hassan Dilunga na Emmanuel Okwi kuwa fit kuelekea mchezo huo.
Mara
baada ya mazoezi ya leo, kocha mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie
Brandts amesema kiufundi ameshamaliza kazi yake na kikubwa anachosubiri
ni kufika hiyo kesho ateremshe kikosi chake dimbani kusaka ushindi ambao
ndio itakua furaha ya wanachama, wapenzi na washabiki wa timu ya Yanga.