Waziri
wa ujenzi John Pombe Magufuli akitoa salamu za rambirambi kwenye ibada
ya mazishi ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Diwani
wa kata ya Kisesa hadi mauti yalipomkuta Marehemu Clement Mabina.
Waziri wa ujenzi John Pombe Magufuli akitoa mkono wa pole kwa familia ya Marehemu Mabina.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akito salamu za rambirambi kwa
niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete
kwenye ibada ya mazishi ya Mabina.
Akitoa
salamu za rambirambi kwaniaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarsti
Ndikilo amesema kuwa, Rais Kikwete ametoa pole kwa wananchi wa Kisesa na
Mkoa wa Mwanza juu ya tukio hili la msiba wa marehemu Mabina (58) na
mtoto Tevery Malemi (12) kutokana na vifo vilivyosababishwa na mgogoro
wa ardhi.
Ameongeza
kuwa migogoro ya ardhi inapaswa kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa
huku hekima na busara zikitumika kushughulikia utatuzi wa migogoro hiyo
badala ya kutumia hasira jambo ambalo siku zote husababisha majonzi na
madhara makubwa kwa jamii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wasira akitoa salamu za rambirambi.
Sehemu ya wanafamilia na viongozi wa Vyama vya siasa na serikali wakishiriki ibada ya mazishi.
Picha zaote kwa hisani ya G Sengo Blog
Ni sehemu tu ya waombolezaji waliofika katika viwanja vya Red Cross kushiriki ibada hiyo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga akitoa salamu za rambirambi.
Mbunge wa Jimbo la Magu naye alitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo.
Katibu
wa uhamasishaji wa Chipukizi UVCCM Taifa Paulo Makonda (kushoto)
alishindwa kujizuia kuficha hisia zake na kububujikwa na machozi, kulia
ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja naye akipiga dua la
kumuombe amarehemu Mabina.
Mkuu wa wilaya ya Magu Jackline Liana akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani humo.
Huku
akibubujikwa na machozi na kuangua kilio, Mbunge wa Jimbo la Magu Festus
Limbu akimpa mkono wa pole mjane wa marehemu Mabina.
Katibu wa uhamasishaji wa Chipukizi UVCCM Taifa Paulo Makonda akiwasilisha salamu za rambirambi.
Askofu
Mstaafu wa kanisa la AICT Paulo Nyagwaswa naye alipata fursa ya kutoa
neno kwa maelfu ya waombolezaji waliojitokeza leo kwenye ibada hiyo ya
mazishi.
Sehemu ya makada wa Chama cha Mapinduzi.
Ulinzi na utaratibu ulizingatiwa na kamati ya mazishi.
Ni
moja kati ya eneo la mti wa historia ndani ya viwanja hivyo ambapo
baadhi ya waombolezaji waliketi wakifuatilia mwenendo wa ibada.
Kusalimiana na kupeana pole kwa viongozi.
Umati ukisubiri kuuaga mwili wa marehemu Mabina.
Uwanjani ilikuwa hivi.
Kutoka juu.
Ndugu
wa karibu na marehemu wakiongozwa na baadhi ya watawa kutoka eneo la
ibada ya mazishi tayarikuelekea eneo la maziko kitongoji cha Kanyama.
PICHA KWA HISANI YA MICHUZI BLOG