kada wa ccm kutoka chuo kikuu cha Iringa Simon Belege akimwaga sera kwa wananchi na kuwaeleza sababu za kuichagua CCM
Kada wa CCM maarufu mjini Iringa Frederick Mwakalebela akiwahutubia wananchi wa kata ya Nduli
vijana wa ccm wakiwa wamenegewa na mkutano na kushindwa kuogopa hata mvua
wananchi wa Nduli wakiendelea kunyeshewa na mvua wakati mkutano ukiendelea(P.T)
viongozi wa CCM wakiendelea kunyeshewa na mvua pamoja na wana Nduli wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo
Katibu wa CCM Iringa mjini Hassan Mtenga akiwahutubia wananchi wa Nduli katika uzinduzi wa kampeni za udiwani kata ya Nduli
Mbunge wa Mufindi kusini Mendrad Kigolla akieleza juu ya fedha za mfuko wa jimbo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akihutubia katka mkutano huo
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa kampeni Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi kulia akimnadi mgombea udiwani wa CCM kata ya Nduli Bw Mtove
Bw Mtove akiwa na wenzake walioingia katika mchakato wa kura za maoni kabla ya kuwashinda
Kada wa CCM Frederick Mwakalebela na Simon Belege kushoto wakiwa katika mkutano huo
Na Francis Godwin Blogu
CHAMA cha mapinduzi ( CCM) wilaya ya
Iringa mjini kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya
Nduli jimbo la Iringa mjini huku katibu wa CCM wilaya hiyo Hassan Mtenga
amemtaka mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman
Mwamwindi kumbana mbunge mchungaji Peter Msigwa ili kuonyesha mamilioni
ya shilingi ambayo anadai yalitolewa na mfanyabiashara Sabodo kwa ajili
ya kusaidia maji wananchi wa jimbo la Iringa wakiwemo wa Nduli.
Mbali ya katibu huyo kumwagiza meya
kufuatilia fedha hizo ili kujua kazi ambayo zilifanya pia Meya Mwamwindi
ameueleza umati mkubwa wa wananchi waliofika katika mkutano huo kazi
chache ambazo anazitambua alizozifanya mbunge Msingwa kwa miaka yake
miwili akiwa mbunge.
Imedaiwa mfanyabiashara Sabodo
mwaka jana alinukuliwa na vyombo vya habari akijitolea fedha za
uchimbaji wa visima vya maji kwa wabunge wote wa majimbo wa CHADEMA
kama njia ya kumaliza kero ya maji majimboni mwao ila hadi sasa
jimbo la Iringa mjini eneo la Kigonzile kata hiyo ya Nduli
wananchi wake wanashida kubwa ya maji.
Mwamwindi alitaja kazi hizo kuwa ni
pamoja na kugawa mipira kata zote 16 isipo kuwa Nduli,kupeleka vitanda
visizo chakavu katika Hospitali ya wilaya ya Iringa mjini (Frelimo)
vitanda ambavyo hadi sasa havitumiki ,pamoja na kutoshindwa kushiriki
vikao vya baraza la madiwani kwa miaka miwili kabla ya kulalamikiwa na
kazi nyingine ambayo amekuwa akiifanya ambayo haina faida kwa wana
Iringa ni kupigania ujangili wa Twiga na Tembo hali akijua jimboni kwake
hakuna hifadhi ya wanyama. Pia Mwamwindi alipongeza jitihada
zinazofanywa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM)
kwa kujenga kituo cha polisi kusaidia ufunguzi wa Hospital ya wilaya ,
kusaidia kusomesha yatima, kuwezesha wanawake kiuchumia na kazi nyingine
nyingi.
Hata hivyo alisema mbali ya kuwa
katika mfuko wa jimbo kuna kiasi cha Tsh milini 30 ambazo zimetolewa na
Rais Jakaya Kikwete ila wajumbe wa mfuko huo wamekuwa wakishindwa
kukutana kutoa maamuzi juu ya fedha hizo kutokana na mbunge kuonyesha
kuwazunguka na kugoma kukaa vikao.
Mwamwindi alisema kuwa serikali ya CCM
katika kata hiyo ya Nduli pekee imefanikisha kusogeza maendeleo kwa
wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja katika kijiji cha Kigonzile
pamoja na kufikisha usafiri wa daladala ambapo toka nchi ipate uhuru
wananchi hao kwa sasa wanapata usafiri , pia kwa nduli ujenzi wa shule
ya sekondari pamoja na kupeleka mradi kubwa wa maji unaogharimu zaidi ya
Tsh milioni 70 mradi ambao mbunge wao amekuwa hauungi mkono kutokana na
kususa siku ya uzinduzi.
Huku kwa upande wake aliyekuwa
mshindi wa kura za maoni katika mchakato wa ndani ya CCM mwaka 2010
Frederick Mwakalebela akiwataka vijana na wananchi wa kata ya Nduli
kumchagua mgombea udiwani wa CCM Bw Benitho Mtove kuwa ndie
atakayefanikisha maendeleo ya jimbo la Iringa na kata ya Nduli.
Akihotubia huku akishangiliwa na umati
wa wananchi waliofika katika mkutano huo Mwakalebela alisema bado
anaheshimu jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya CCM chini ya rais
Kikwete na kuwa ili kasi ya maendeleo iendelee kuwepo wananchi wa Nduli
hawana budi kuchagua CCM na sio kuchangua mpinzani.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca
Msambatavangu aliwataka wananchi wa Nduli katika kumuenzi diwani
aliyefariki duni Idd Chonanga kutobabaika na kauli za Msingwa na badala
yake kuchagua diwani wa CCM.
Hata hivyo mgombea huyo wa udiwani Bw
Mtove ambae hakutaka kumzungumzia mbunge Msigwa wala mgombea wa Chadema
udiwani katika kata hiyo ,alisema anahakika atafanya kazi ya kuwatumikia
wananchi wa Nduli na kuomba tarehe 9 kumpa kura zote za ndio.