| wafanyabiashara Iringa wakiwa katika mgomo eneo ya Miyomboni leo |
| Maduka Miyomboni yakiwa yamefungwa leo |
| Wateja wakiwa wamekwama kupata huduma le |
| Maduka mbali mbali ya mjini Iringa yakiwa yamefungwa leo |
| Wafanyabiashara eneo la stendi ya Miyomboni wakiwa wamesimama nje ya maduka yao leo |
Mfanyabiashara Erick Makofia akipita eneo la Miyomboni leo ...................................................................................................
HALI ya swari katika mji wa Iringa kufuatia kuanza kwa mgomo usio na kikomo wa wafanyabiashara kama njia ya kufikisha ujumbe kwa waziri wa fedha na serikali ya Rais Jakaya Kikwete juu ya gharama za mashine za EFD
Mgomo huu umeanza leo asubuhi hii katika mjini wa Iringa huku wakipanga kufanya maandamano kuwaadhibu wenzao wanaokiuka mgomo huo.
Hali kwa upande wa wakazi wa Iringa mjini na wale wa maeneo na wilaya na mji mingine wanao kuja kwaajili ya kupata huduma imewapa wakati mgumu kutokana na mgomo huo, hivyo kujikuta wakiambulia makufuri katika maduka
Hata hivyo wafanyabiashara hao wametoa onyo kwa wenzao iwapo watafungua maduka yao watakiona cha moto na kuwa kuanzia wakati wowote sasa wataanza msako wa duka moja hadi jingine kwani amesema mgomo huo ni nchi nzima na wao wametii uamuzi wa wafanyabiashara wa jijini Dar es Salaam ambao pia wapo katika mgomo kama huo
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma amewaangukia wafanyabiashara hao kwa kuwataka kutoaendelea na mgomo huo bali kuendelea na biashara hata kama bila mashine hizo wakati serikali ikitafuta suluhu ya suala hilo.
Akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com kwa njia ya simu Dr Ishengoma alisema kuwa si busara kwa wafanyabiashara hao kugoma kwani toka awali si wote walikuwa na mashine hizo na bado waliendelea kufanya shughuli zao.
" Mbona siku zote walikuwa wanauza bila mashine na hadi sasa hakuna mfanyabiashara aliyekamatwa kwa kukosa mashine....nawaomba wafungue maduka yao"
Wakati kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi akiwataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu na kuwa atakayefanya vurugu jeshi la polisi litachukua hatua kali dhidi yake na kuwa jeshi hilo limejipanga kwa ulinzi .
CHANZO:Mzee wa Matukio Daima.
Post a Comment