Victor Anichebe akipiga kichwa na kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Chelsea katika mechi iliyochezwa jana katika Uwanja wa Hawthorns(Picha na BBC SPort)
......
Chelsea imepoteza nafasi ya kuhakikisha kuwa imesalia
kileleni mwa ligi kuu ya Premier ya Uingereza, mbele ya mahasimu wao
Arsenal, baada ya kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na West
Brom, katika mechi iliyochezewa katika uwanja wa Hawthorns.
Victor Anichebe aliifungia West Brom bao hilo
muhimu kunako dakika ya 87 Na kuinyima Chelsea alama mbili ambazo
zingeihakikishia Chelsea hakikisho la uongozi wa ligi hiyo hadi juma
lijalo.
Branislav
Ivanovic aliiweka Chelsea mbele dakika ya 45, bao ambalo lilikuwa
limeipa vijana hao wa Jose Mourinho kuwa alama nne mbele ya Arsenal
ambayo kwa sasa inashikilia nafasi ya pili.

Post a Comment