James Collins wa West Ham akiruka juu na na kuifungia timu yake goli dhidi ya Norwich na kuihakikishia timu yake pointi tatu muhimu.
,,,,,,,,,,,,
West Ham imepanda hadi nafasi ya kumi kwenye jadwali ya ligi hiyo baada ya kuilaza Norwich kwa magoli mawili kwa bila.Magoli ya James Collins na Mohamed Diame yalitosha kuipa timu yao pointi tatu muhimu.
Ushindi huo ulikuwa wa tatu mfululizo kwa timu hiyo iliyo na makao yake Mashariki mwa jiji la London.
Norwich kwa upande wake inashikilia nafasi ya
kumi na sita alama moja mbele ya West Brom na Sunderland iiliyo katika
nafasi ya kumi na saba na kumi na nane mtawalia

Post a Comment