Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MGOMO WAINGIA SIKU YA PILI LEO ARUSHA


10945926_10206209432461067_618369046_n
10945148_10206209432101058_86714147_n
10942264_10206209425620896_109277478_n Wanafunzi wakilazimika kutembea kwa miguu kuelekea shuleni kutokana na mgomo wa daladala maarufu kama 'vifodi' ulioingia siku ya pili leo kwa baadhi ya njia.
10934633_10206209425380890_1698646785_n
10934354_10206209417460692_719586644_n
10943120_10206209417660697_2019217090_n
10943166_10206209478102208_404477145_n
10917757_10206209432741074_1219896982_n

Wananchi wakitumia gari za mizigo ili kuwahi makazini kutokana na mgomo wa vifodi ulioanza jana na kuingia siku ya pili leo .
10847140_10206209478702223_1921904825_n
10721199_10206209649306488_50490285_n
Kile kinachotafsiriwa kuwa mgomo wa waendesha magari madogo ya kubeba abiria kwa Jiji la Arusha maarufu kama “vifodi” umeendelea tena hii leo ikiwa ni siku ya pili mfululizo kwa baadhi ya njia.

Kwa mfano kwa njia ya kutoka maeneo ya Moshono kuelekea mjini hakuna gari yeyete ya abiria kabisa, halikadhalika njia itokayo Njiro kwenye mjini pia. Wasafiri wa njia hizo wamejikuta wakilazimika kusafiri katika mazingira ya hatari kwa kujazana kwenye magari ya wazi na pikipiki za mizigo vyombo ambavyo si maalumu kwa ubebeaji wa abiria. 

Uchunguzi wa Blog hii umegundua kuwa wanaosababisha zaidi hali hii ni wapiga debe ambao wanaona kwa mfumo mpya wa hizi njia za usafiri kama mpango wa Jiji kukabiliana na msongamano barabarani hawataweza kupata ujira wa kuitia abiria kwenye magari, na hivyo baadhi yao kuwafanyia vurugu madereva wanaotaka kufanya kazi. 

Lakini pia kuna baadhi ya madereva ambao ni kama hawauelewa utaratibu huo mpya na kujikuta wakigoma kuendesha magari yao. 

Habari kwa hisani ya Arusha255
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top