
WAKAZI wa
jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa wameiomba Kampuni ya Msama Promotions
inayoandaa Tamasha la Pasaka na Krismasi kuwapa nafasi ya upendeleo kwa
kuwapelekea tamasha katika mkoa huo.
Sababu za
kupewa kipaumbele katika Tamasha la Pasaka mwaka huu ni baada ya
kulikosa Tamasha la Kirismasi ambalo lilifanyika kwenye mikoa ya Mbeya,
Iringa na Songea .
Kwa
mujibu wa wakazi hao ambao waliwaomba waandaaji wa matamasha hayo ya
injili, Kassim Mtolea mwanafunzi wa Chuo cha SAUT wanamuomba Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotions Alex Msama na kamati yake kuwafikiria kwa
sababu linashirikisha waimbaji wa Kimataifa.
Mtolea
alisema wanamuomba Msama kuwafikiria zaidi kwa sababu miaka yote tangu
limeasisiwa limekuwa likianzia jijini Dar es Salaam hivyo ni vyema
waandaaji wakabadilika na kulipeleka kwanza Jijini Mwanza.
Aniceth
Nyahore ambaye ni mkazi wa Maswa lalieleza kuwa iwapo tamasha hilo
litaanzia Mwanza litakutanisha mikoa ya Geita, Shinyanga, Mara na Kagera
katika uwanja wa CCM Kirumba na kueneza injili pamoja na burudani.
Nyahore
alisema ubora wa Matamasha hayo unatokana na ushiriki wa waimbaji wa
Kimataifa wanaotoka nchi za Afrika Kusini, Kenya, Uganda, Rwanda na
Uingereza ambao umekuwa ukivutia umati mkubwa wa mashabiki.
Daniel
Mkate aliishauri Kamati ya maandalizi kuzingatia kuanza na mkoa wa
Mwanza baada ya kulikosa Tamasha la Krismasi lililofanyika mwaka jana
huku wakazi hao wakiwa na kiu kubwa.
Sambamba
na kuliomba tamasha hilo mkoani humo pia aliishukuru Kamati ya
Maandalizi kwa kumleta muimbaji Rebecca Malope ambaye alishiriki tamasha
la mwaka juzi.
Aidha
Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alikiri kupokea
maombi haya ambapo alisema ni vigumu kutoa maamuzi maana bado ni mapema
mno, lakini aliahidi kuyafanyia kazi.
Habari na VICTOR SIMON Mjengwa Blog
Post a Comment