Mkurugenzi
M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu akifafanua jambo kwa
waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi za Afrika
waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali
vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice hivi
karibuni nchini Mauritius.
Mkurugenzi
wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus akifurahi
jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi
mbalimbali za Afrika.
Na Modewjiblog, Mauritius
Moja
ya makampuni yanayoongoza katika utoaji wa vipindi vya burudani barani
Afrika M-Net imesema kwamba itazindua chaneli maalumu kwa ajiri ya
wakazi wa Tanzania itakayojulikana kama maisha Magic Bongo.
MAISHA
MAGIC BONGO itaruka hewani kupitia chaneli 160 ya DStv kuanzia Alhamisi
ya Oktoba Mosi mwaka huu na itapatikana katika vifurushi vyote
vya Access, Family, Compact, Compact Plus na Premium.
Imeelezwa
kuwa ingawa mambo yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya Watanzania
mataifa jirani yaAfrika Mashariki ikiwamo Kenya, Uganda, Ethiopia na DRC
wanaweza kuona.
Uamuzi huo wa M-Net umefanyika wakati mchakato unaendelea wa kuboresha zaidi ulaji kwa wateja wake.
Hata
hivyo wamesema kwamba MAISHA MAGIC EAST ambayo kwa sasa inaruka kupitia
chaneli 158 itajiimarisha zaidi katika soko la Kenya huku ikiendelea na
mara moja kwa wiki kwa ajili ya soko la Uganda ndani ya Luganda.
Pichani
ni waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliokusanyika
kwenye jukwaa hilo lililoandaliwa na MultiChoice Africa hivi karibuni.
MAISHA
MAGIC BONGO imelenga kuhudumia soko la Tanzania likionesha vipindi vya
Kiswahili kwa ajili ya kutimiza pia lengo la taasisi la kuhudumia soko
kwa kuangalia makundi.
Mkurugenzi
wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus amesema
ingawa kwa miaka mingi wamekuwa wakitoa vipindi vyenye lugha
mchanganyiko kwa sasa wamepania kutoa vipindi kwa lugha ya eneo kutokana
na soko kuruhusu.
“Tumefanya
mabadiliko kwa nchi za Afrika Mashariki kwa siku za karibuni. Kasi ya
mabadiliko hayo yanaonesha kujali kwetu. Na tutaangalia mafanikio
katika MAISHA MAGIC BONGO, kuona uwezekano wa kuendelea kutengeneza
chaneli zinazokidhi mahitaji Fulani.” Amesema Erasmus.
Chaneli
mpya itakuwa na matangazo ya saa sita ambayo yatarejewa mara tatu kwa
siku na inatarajiwa saa za vipindi kuongezeka zaidi.
Katika
chaneli hiyo kutakuwa na kipindi cha saa moja cha muziki Mzooka, ambayo
itakuwa mwishoni mwa wiki majira ya jioni na itakuwa kipindi cha miziki
ya karibuni kutoka Tanzania. Kitakuwa ni kipindi cha wapenzi wa hip hop
na Bongo.
Mkurugenzi
M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na Movie Stars wa nchini Nigeria, Rita Dominic na
Desmond Elliot mara baada ya mkutano na waandishi wa habari.
Pia
kutakuwa na michezo ya kuigiza ambayo ni tamthilia Talaaka itakayokuwa
ikizungumzia masuala ya ndoa na talaka na kupeleka ujumbe kwanini
kunakuwa na talaka. Pia kutakuwa na kipindi cha mapishi cha Jikoni na
Marion. Kwenye kipindi hiki tutawaona masupastaa wa Tanzania wakipika
chakula huku wakizungumzia mambo yao.
MAISHA
MAGIC BONGO kutakuwa na sinema za Kiswahili kama Nusra iliyochezwa na
Ashura Iddy, Ammar Ruweth, Riyama Ally na Zuberi Mohammed. Pia kutakuwa
na sinema ya Hard Price iliyochezwa na akina Sabrina Tamim na Jacqueline
Wolper .
Ikiwa
imebaki mwezi mzima kabla ya MAISHA MAGIC BONGO kuingia katika runinga
za watanzania kwa sasa angalia kipindi gani kipo hewani ukipendacho
kupitia www.dstv.com.
Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic, Margaret Mathore akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Post a Comment