Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu
zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa
kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya
rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda nafasi ya Urais.
Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli
alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka
huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka
mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
Dkt
Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la
Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni
uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye
mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja
wa Samora mkoani Iringa.
Magufulika
staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa
nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo
jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa
wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi
hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga
push up kama ionekanavyo pichani.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo
Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani
Iringa.
Dk
Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Ndugu
Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Ifunda
Vimbwanga vya hapa na pale vilikuwepo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ifunda mapema leo mchana
wazee
wa kimila wa kabila la Wahehe wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt
Magufuli uliofanyika mapema leo mchana katika Mji wa Ilula Jimbo la
Kilolo mkoani Iringa.
Mjumbe
wa Kamati ya Kampeni za CCM, William Lukuvi akitangaza wasifu wa
mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli wakati wa mkutano wa
kampeni kwenye Uwanja Samora mjini Iringa.
Wananchi
wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Samora wakisikiliza sera za
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
Wananchi
wa Iringa na vitongoji vyake wakifuatilia mkutano wa kampeni,wakati Dkt
Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba
25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze
kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
Baadhi
ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven
a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi
sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu
kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika
mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao
tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale
wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.PICHA ZOTE NA MICHUZI
JR-IRINGA
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa
Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani
Iringa.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa
Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani
Iringa.
Post a Comment