Na Bashir Nkoromo
Mgombea Mwenza wa Urais kw tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, leo anaanza ziara ya kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa wa Morogoro.
Mama samia ambaye anaanza mkoa wa Morogoro akitokea Dodoma ambako alipumzika kwa ajili ya Sikukuu ya Eid El Hajj, kulingana na ratiba iliyopo, leo atafanya mikutano Gairo, Dumila, Kilosa na Mikumi.
Kabla ya mapumziko mkoani Dodoma, Mama Samia alitoka kufanya mikutano ya kampeni katika mkoa wa Tanga, Manyara na wilayani Kondoa.
Post a Comment